Kikundi kinachodaiwa kuwa Panya Road wametikisa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na kupora vitu, kujeruhi watu wakiwa na mapanga mikononi mwao maeneo ya Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku wa leo. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Fujo zaidi zilianzia mchana leo wakati kiongozi wao aitwaye Diamond alipouawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzao leo wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo. Kilichotokea, polisi walikuwa eneo hilo tena ndani ya difenda kwa ajili ya kuhakikisha kuna amani wakati wa maziko.
Maziko yalipokwisha, vijana hao wakatawanyika, ila baadae wakaanza kujikusanya na kuanza kuleta fujo tena baada ya kuhakikisha kwamba polisi wameondoka.
0 comments:
Post a Comment