PROFESA LIPUMBA NA WAFUASI WA CUF WAPIGWA MABOMU NA POLISI NA KUKAMATWA
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama
cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa
Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.
Awali
polisi ilizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya
kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso
ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.
Akizungumza
leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema
wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30
ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili
ya mahojiano.
“Wanachama
32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati
kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea
kuwahoji,”alisema Siro.
Siro
alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho
hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa
kuhofia fujo kutokea.
Siro
alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa
mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya
polisi na wananchi kufa.
“Jeshi
la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na
hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano
hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.
Alisema
sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni
walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na
mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia
kutokea mambo mabaya.
Kufuatia hali hiyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeshtushwa na kupigwa vibaya na kukamatwa Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof Ibrahim Lipumba
Tayari Uongozi wa juu wa CHADEMA pamoja na mawakili wa chama wameelekea Police Central Station kwa ajili ya tukio la kijahili walilofanyiwa viongozi wa CUF, Profesa Lipumba na wengine.
Lengo la mawakili wa Chadema ni kuhakikisha wanamtoa kwa gharama yoyote Prof Lipumba na wanachama wote wa CUF waliokamatwa.
Tayari Uongozi wa juu wa CHADEMA pamoja na mawakili wa chama wameelekea Police Central Station kwa ajili ya tukio la kijahili walilofanyiwa viongozi wa CUF, Profesa Lipumba na wengine.
Lengo la mawakili wa Chadema ni kuhakikisha wanamtoa kwa gharama yoyote Prof Lipumba na wanachama wote wa CUF waliokamatwa.
0 comments:
Post a Comment