Wagombea Udiwani Watakiwa Kupima Virusi Vya Ukimwi Kabla ya Kuchua Fomu za Kugombea
MADIWANI wa Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi wameshauriwa kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kabla ya kuchukua fomu za kugombea nafasi ya udiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Diwani
wa kata ya Kapalala, Reward Sichone alitoa ushauri huo katika kikao cha
Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudhibiti Ukimwi, Diwani wa kata ya Sitalike, Silvester Nswima
kuwasilisha taarifa kuhusu hali ya Ukimwi.
Hata
hivyo Nswima alipinga ushauri huo wa Sichone, akisema suala la madiwani
kupimwa afya zao kwa pamoja haiwezekani, kwani kupima ni hiyari ya kila
mtu na si lazima, hivyo kila mtu atapima kwa muda wake na kwa hiyari
yake.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Nsimbo, Mohammed Assenga alisema kitendo cha madiwani
kupima afya zao kinaweza kuwa ni mfano mzuri kwa watumishi na wananchi
wa Halmashauri ya Nsimbo.
0 comments:
Post a Comment