KENDO..!! MANESI WADAIWA KUMTUMBUKIZA MTOTO KWENYE NDOO AKIWA HAI, BAADA YA MAMA KUJIFUNGUA HUKO MOROGORO
HOT NEWZZZZZZZZZZ HII NI NOMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Mama wa mtoto huyo, Zainabu lsmali
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Manesi wa
wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wameingia
kwenye kashfa nzito ya kusababisha kifo baada ya kudaiwa kumtumbukiza
mtoto mchanga kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.
Tukio hilo ambalo kwa
sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye
Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha
Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua na kukimbizwa katika
hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha kwa jina la
Mama Sira Manga.
Ndoo iliyotumika.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda juu ya tukio hilo, Mama Manga alikuwa na
haya ya kusema: “Huu ni uzembe mkubwa wa manesi. Tulipofika hospitali
mtoto alizaliwa akiwa hai lakini alikuwa njiti kwani alikaa tumboni kwa
mama yake miezi 7 badala ya 9.
Ndugu wa mama akiwa na mtoto huyo.
“Cha ajabu usiku huo
manesi baada ya kumcheki mtoto walisema ni wa kike lakini eti walidai
amekufa hivyo waliamua kuchukua matambara ya mzazi yaliyotumika
kujifungua na kumzoa mtoto huyo na kumuweka kwenye ndoo ambayo kwa
kawaida sisi wazazi huwa tunakwenda nazo leba.
“Walituambia tukazike,
unajua kutoka hospitali hadi Kididimo juu ya Milima ya Uluguru ni mbali
na gari lilichelewa kutufuata hivyo mtoto huyo alikaa kwenye ndoo zaidi
ya saa 3.
“Tulipofika nyumbani na
kumtoa mtoto kwenye ndoo tukamuona anahema na kufumbua macho baada ya
kumtingisha akakohoa ndipo tukamkimbiza tena hospitali.
Pamoja na jitihada za
manesi hao, kesho yake mtoto huyo alifariki dunia baada ya kitovu chake
kuingiza hewa kwani kilikuwa bado hakijakatwa.
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:
“Roho inauma sana lakini mzungumzaji wa tukio hilo ni mume wangu.”
Baba wa mtoto huyo, Haji
Kondo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema: “Ni kweli nimempoteza
mwanangu lakini nisingependa kutoa lawama kwa manesi kwani mke wangu
bado anaendelea kuzaa.”
Mwandishi wetu alifika
hospitalini hapo na kuzungumza na daktari mfawidhi, Dokta Rita Lyamuya
ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dokta Rita Lyamuya.
“Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye wodi yetu ya wazazi.
“Manesi walitimiza jukumu
lao la kumhudumia mzazi lakini kwa bahati mbaya tuna changamoto ya
umeme kukatika bila taarifa hivyo wakati manesi wakimzalisha alijifungua
mtoto njiti.
“Ghafla umeme ulikatika
na kutokana na giza, manesi walijua mtoto amekufa hivyo waliwaeleza
wanandugu kwamba mtoto amefariki dunia.
“Ndugu walimchukua walipofika kwao na kukitoa kwenye ndoo walibaini mtoto bado yupo hai.
“Walimleta tena hapa hospitali na tulifanya juhudi za kumtibu lakini kwa bahati mbaya amefariki dunia.”
0 comments:
Post a Comment