Tukio limekamilika kwenye Uwanja wa
Uhuru, Temeke Dar es Salaam… ni historia nyingine iliyoandikwa kwa Rais
JK kukabidhi kijiti cha Urais kwa Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Hapa ni Rais John Pombe Magufuli akiwa anakula kiapo.
“Mimi John Joseph Pombe Magufuli, naapa nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nitalinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria, ewe Mwenyezi MUNGU nisaidie.” >>> Rais John Joseph Pombe Magufuli.
“Mimi John Joseph Magufuli
naapa nitatenda kazi zangu za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa uaminifu kwa kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo
mkunjufu na nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Sheria, mila na
desturi za Tanzania, bila woga, bila upendeleo, huba wala chuki… ewe
mwenyezi MUNGU nisaidie.” >>> Rais JPM.
“Mimi John Pombe Magufuli
naapa katika kutekeleza majukumu katika kutekeleza madaraka niliyopewa
kwa mujibu wa KATIBA ya Umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
nitatetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
mujibu wa Katiba, ewe Mwenyezi MUNGU nisaidie.” – Rais JPM.
Baada ya hapo kikafuatia kiapo cha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan >>>
“Mimi Samia Suluhu Hassan,
naapa nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
nitalinda na kuitetea KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria, ewe Mwenyezi MUNGU nisaidie.”- Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
“Mimi Samia Suluhu Hassan
naapa nitatenda kazi zangu za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa uaminifu kwa kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na
moyo mkunjufu na nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Sheria, mila
na desturi za Tanzania, bila woga, bila upendeleo, huba wala chuki… ewe
mwenyezi MUNGU nisaidie.” >>>
“Nitaitumikia vyema Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika kazi yangu ya Makamu wa Rais na wakati wote
nitamshauri kwa hekima na uaminifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, vilevile sitatoa siri za Baraza la Mawaziri, ewe Mwenyezi
MUNGU nisaidie.” >>> Mama Samia Suluhu.
“Mimi Samia Suluhu Hassan
naapa kwamba katika kutekeleza madaraka niliyopewa kwa mujibu wa Katiba
ya Tanzania, nitatetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa mujibu wa Katiba, ewe Mwenyezi MUNGU nisaidie.” >>> Mama Samia Suluhu.
0 comments:
Post a Comment