Maneno ya mke wa Marehemu wiki tatu baada ya msiba wa Deo Filikunjombe.
Tanzania bado iko kwenye majonzi baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo Haule Filikunjombe pamoja na Rubani Captain William Silaa na watu wengine wawili Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule waliofariki kwenye ajali ya Helikopta kwenye mbuga ya Selous.
Marehemu Deo Haule Filikunjombe ameacha mke na watoto, ambapo siku chache zilizopita kupitia kwenye akaunti ya instagram mke wa marehemu Filikunjombe, Saraha ameyaandika kuhusu vitu ambavyo vilikuwa vikizungumzwa hasa kwenye mitandao mbalimbali.
‘Za siku wapendwa nawashukuru wote kwa text nyingi za pole mlizonipa na kuwa pamoja na familia yangu kwa kipindi hiki kigumu kwetu kwa kumpoteza mtu muhimu katika maisha yangu nilizoea kumuita majina mazuri yote ila yale yote ntayahamishia kwa wanangu ulioniachia nawahakikishia nitasimama sehemu zote mbili kama baba na kama mama nitakupenda daima mume wangu Deo wangu Filikunjombe wangu jembe langu
0 comments:
Post a Comment