Taasis za umma zilivyojipanga kutekeleza maagizo ya Rais MAGUFULI…

Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli ameendelea na operesheni yake ya kuhakikisha anaondoa matumizi yasiyo ya lazima katika taasisi mbalimbali za Serikali.
Ukiachia kufuta safari zisizo za lazima kwa watumishi wa umma tayari amewaondoa baadhi ya watendaji ambao wamekutwa na makosa mbalimbali yaliyoliletea Taifa hasara.
Leo makampuni mbalimbali ya umma na taasisi za Kiserikali zimekutaka katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam kuzungumzia mikakati yao kufuati agizo la rais la kuondoa matumizi yasiyo ya lazima.
Lawrance Mafuru ambaye ni msajili wa hazina amezungumza na viongozi mbalimbali wa makampuni na kusema “Kila mtu ambaye yupo kwenye eneo la kutoa huduma kwa jamii anatakiwa kuhakikisha anaondoa kero kwenye huduma zake, tujifunze kutoka katika makampuni binafsi”.
“Tuna benki za kutosha kama Serikali, tumenunua mabehewa lakini tumefuata utaratibu? inashangaza kuona ni mabovu,,wamekagua lakini bado wameletewa mabehewa mabovu, wale wote mliopewa nafasi kusimamia makampuni makubwa kama haya”.Lawrance Mafuru
List ya mikakati tunayotakiwa kufanya kwenye taasis zenu…“Makatibu wakuu waliitwa na Rais na kupewa maelekezo mbalimbali, tunapaswa kufanya majukumu yetu kwa ufasaha, kama unatakiwa kutengeneza umeme utatakiwa kufanya kwa wakati..Serikali na taasis zake ifanye kazi pamoja, kila mmoja aheshimu mamlaka na nafasi ya mwingine”.
“Taasisi ambazo zina kazi ya kutoa huduma kwa jamii mfano maji, umeme zifanywe kwa sera zilizopo, hawatakiwi kujazana hazina wakidai hawana pesa, wanatakiwa kutafuta namna ya kuendeleza miradi yao, tutaipa Serikali changamoto ya kuongeza mitaji,,sio kila kitu lazima tufanye na wageni, tuitumie Serikali kwa moyo”.

3X6A9605
Baadhi ya viongozi wa makampuni waliyohudhuria semina hiyo.
Baadhi ya kampuni hazifanyi ukaguzi wa mahesabu“Ukiwauliza kwa nini wanasema hawana fedha, hakutakuwa na msamaha kama kampuni inashindwa kufanya odit kwa miaka zaidi ya mwaka mmoja, tutamtaka CAG aongeze ukaguzi, na zile kampuni zinazodai hazina pesa zijitokeze na kujieleza”..

Rais Magufuli kaamua Bilioni zilizokua zitumike sherehe za uhuru 9 Dec matumizi yake yawe kama ifuatavyo.


Kwa sababu tayari Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kwamba sherehe za Uhuru siku ya December 09 2015 hazitokuwepo, ninayo taarifa nyingine kuhusu maamuzi mengine ya pesa ambazo zilitengwa kwa shughuli hiyo.
Taarifa kutoka Ikulu imetolewa kwamba fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kutumika kugharamia sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika December 09 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco iliyopo Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia za barabara za lami.
Taarifa hiyo ya Ikulu imesema tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
Hii hapa taarifa yote ya Ikulu.
IMG-20151130-WA0042

Hakitupwi kitu hapa !!… zile chupa unaziona takataka, Nigeria wamejengea mpaka nyumba.. (+Pichaz)


Maisha yanabadilika kila siku, zamani ilikuwa ukikutana na chupa au makopo ya maji au juice unayaona takataka… sasahivi ni dili na watu wameweka nguvu zao kabisa kukusanya makopo na kuyauza !!
Nigeria wamefanya kitu kingine zaidi mtu wangu, umewahi kuona nyumba za makopo??!! Nigeria wamefanya kitu hicho, wamejenga nyumba kwa makopo ambapo ndani ya makopo hayo kumejazwa mchanga halafu makopo yanapangwa vizuri kabisa mpaka inakuwa nyumba ya kuishi.
House3
Sifa nyingine kubwa za hizi nyumba ni kwamba zina uwezo wa kuzuia risasi na pia zinaweza kuzuia moto.
Naija
Kazi ya ujenzi inaendelea namna hii, hatua kwa hatua!!
House4 House6 House7 House8
Unaweza kuwa na swali kwamba chupa kiasi gani au chupa ngapi zinatosha kukamilisha mjengo??!! Jibu lake ni hili hapa, kama unahitaji nyumba ya vyumba viwili inatakiwa kuwepo na chupa 14,000… Umevutiwa na ujenzi wa aina hii mtu wangu ???

Matatu niliyoyapata kwenye hukumu ya Sheikh Ponda Morogoro leo…

Hii taarifa tayari imeripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vingi vya habari kutoka Mkoa wa Morogoro ambapo inahusu kutolewa kwa hukumu ya Sheikh Issa Ponda ambaye ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia.
Sheikh Issa Ponda alishtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kukiuka amri ya Mahakama kufanya mkusanyiko pamoja na kutoa maneno ya uchochezi… Mawakili wa Sheikh Issa Ponda wamesema waliamini haki itatendeka japo imechelewa.
Baada ya hukumu hiyo, Sheikh Ponda aliondoka kuelekea kwenye Msikiti wa ‘MUNGU Mmoja Dini Moja‘ uliopo Morogoro kwa ajili ya kuongea na waumini wake.

MSIKILIZE KAMANDA MUNGI HUYU HAPA BONYEZA PLAY


WAWILI WAFARIKI DUNIA MKOANI IRINGA KATIKA MATUKIO TOFAUTI LIKIWEMO LA MMOJA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI



Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la mtu mmoja mkazi wa mtwivila kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulkana manispaa ya iringa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa iringa RPC RAMANDANI ATHUMANI MUNGI amesema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la TRM Minyarani kata ya mkimbizi.

Katika tukio la pili kamanda MUNGI ameongeza kuwa mtu mmoja amefariki dunia katika ajali baada ya kugongwa na pikipiki eneo la mnazi mmoja kata ya Kitwiru.

Awali kamanda mungi ameongeza kuwa jeshi la polisi  linaendelea na uchunguzi ili kuwakamata waliohusika kufanya mauaji ya JEOPHREY HARDSON.


MSIKILIZE KAMANDA MUNGI HAPA BONYEZA PLAY.

Waziri Mkuu: Tumedhamiria Kuwatumikia Watanzania...Tutahakikisha Mapato Ya Taifa Yanatumika Kwa Maslahi ya Watanzania Wote

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.

Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida.
 “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015. 

“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,”
 aliongeza.

Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti. 


Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi. 

Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu.
 
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,”
alisisitiza.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.

Lowassa, Mbowe Watua Alipouawa Alphonce Mawazo


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe  na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho Mhe. Edward Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo alifanyiwa kitendo ya kinyama cha kukatwakatwa mapanga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CCM ikiwa ni umbali mchache kutoka kutuo cha polisi na ofisi za CCM katika barabara kuu inayoelekea Geita kutokea Busanda. 
Umati mkubwa wa wakazi wa Jimbo la Busanda waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mgombea ubunge na M/kiti wa Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Mwili wa Marehemu Alphonce mawazo ukipokelewa na wakazi wa jimbo la Busanda ambako alikuwa akiwania Ubunge katika jimbo hilo

Magazeti ya Tanzania November 30 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC02882
.
.
.
.
.
.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog