DAVID ROBERT: Mkali wa Injili anayetesa Channel O na MTV base


KATIKA miaka ya nyuma muziki wa Injili ulidharaulika sana na mtu alipoonekana akiimba muziki huo alionekana kama kituko kwa sababu hakuna aliyekuwa anaguswa na nyimbo hizo.


Si kwamba kipindi hicho hapakuwa na waimbaji wazuri wa muziki huo, la hasha walikuwepo tena waliokuwa wanafanya vizuri pengine kuliko waimbaji wa leo wanaoimba nyimbo za Injili.
Katika miaka hiyo kulikuwa na waimbaji kama Ephraim Mwansasu, Faustine Munishi, Mungu Four, Ency Mwalukasa, Jeniffer Mgendi na baadaye akajitokeza mwimbaji kama Cosmas Chidumule aliyekuwa anapiga muziki wa dunia kabla hajageuzia kibao kwenye nyimbo za injili.
Miaka hiyo ilikuwa ni mara moja sana kusikia muziki wa injili ukipigwa katika kumbi za starehe kama baa, kwenye harusi na mahali pengine kwenye starehe.
Lakini leo hii upepo umebadilika ndivyo alivyoanza kusema mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili nchini, David Robert, aliyeibuka katika anga la muziki huo mwaka 2002 na albamu ya Baba.


Katika albamu hiyo Robert ambaye ana sauti nzito alishirikiana vema na Godwin Gondwe mtangazaji wa ITV ambaye naye ana sauti ya zege au sauti nzito lakini yenye mvuto sana na kuifanya albamu hiyo kuwa na mvuto wa kipekee na kuweka imara katika anga la muziki huo.
Albamu hiyo iliyokuwa na nyimbo kumi iliwashika wengi na kila mpenzi wa nyimbo za injili kupenda kusikiliza nyimbo zilizokuwemo. Baadhi ya nyimbo zilizokuwamo katika albamu hiyo ni Baba, Niongoze, Ngulujangu iliyoimbwa kwa kinyakyusa na nyinginezo.
Kufanya vizuri sokoni kwa albamu hiyo kulikuwa kama kumemtoa kimasomaso Robert kwani mwaka 2003 aliingia studio na kufyatua albamu ya pili inayojulikana kwa jina la Kiganjani pa Mungu.


Albamu hiyo ambayo nayo ilibahatika nayo kufanya vyema katika tasnia ya injili na hivyo ikamlazimu Robert kurekodi video ambayo nayo ilibamba.
Albamu yake ya tatu ni Adui yangu ilikuwa na nyimbo nane, hakuna asiyejua kila kitu kinachotengezwa kwa ubora, hutumia gharama kubwa kukikamilisha.
Hata hivyo Robert alikaa na kutafari, kwa makini jinsi gani anaweza kurekodi video ambayo inaweza kuwa tofauti na video zilizotangulia. Jibu lake lilionekana kuwa ni kujiweka sawa katika fungu la fedha.


Robert aliamua kuzichambua nyimbo zilizo katika albamu hizo mbili na kufanikiwa kurekodi albamu moja aliyoipa jina la 'The Best Of David Robert'.
Mwanamuziki huyo anaeleza kuwa albamu hiyo ilirekodiwa katika mandhari ya kuvutia na mtaalamu wa masuala ya filamu kutoka nchini Ujerumani Daniel Uphaus kwa kushirikiana na Sye ambaye ni mtaalamu wa kuongoza filamu.
Wataalamu hao waliirekodi kwa makini albamu hiyo hali iliyopelekea kukubalika katika soko la kimataifa, ambapo tayari vituo vya Chanel O na Mtv Base waliiomba kwa ajili ya kuirusha katika runinga zao.
Ubora wa albamu hiyo ya The Best of David Robert umetokana na maandalizi ya miaka mitatu aliyoyafanya kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia studio na kutoa kitu hicho ambacho kinamvuto mkubwa.
Kukamilika kwa albamu hiyo kulichukua miezi minne na baada ya kurekodiwa aliipeleka kwa wataalamu wengine kabla ya kuingia sokoni. Katika kuhakikisha albamu hiyo inakuwa tofauti na albamu nyingine hasa za muziki wa injili nchini, Robert alisafiri mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata picha nzuri kutokana na ujumbe wa nyimbo husika.
Mikoa aliyofanikiwa kwenda kurekodi albamu hiyo ni Morogoro, Iringa, Arusha, Moshi, Pwani na Dar es Salaam.


Robert aliyezaliwa Machi 18, mwaka 1978 Mabatini, jijini Mbeya anasema kuwa huduma ya uimbaji alianza tangu akiwa mtoto, alipokuwa shuleni, ambapo aliifanya kwa nguvu zote kwa kutembelea shule mbalimbali kwa lengo la kutoa injili kwa njia ya nyimbo hiyo ikiwa mwaka 1998 wakati akisoma Shule ya Sekondari ya Jitegemee, jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuipenda huduma hiyo wapo waimbaji waliomvutia akiwamo Mchungaji Ephraim Mwansasu, Mchungaji Daniel Richard Mwansumbi na Cosmas Chidumule hao ndio waliompa hamasa kubwa Robert kujikita katika anga la muziki huo wa injili.


Waimbaji hao ndio walikuwa wakimvutia kutokana na sauti zao kuwa nzuri pamoja na ujumbe wa nyimbo uliokuwamo ndani ya nyimbo zao na mitindo waliyokuwa wakiitumia.
Kwa upande wa mafanikio kupitia muziki huo wa Injili Robert anaseama: “Nimefanikiwa kujenga nyumba nzuri ya kisasa, kumiliki gari lakini mafanikio mengine ni pamoja na kupata mtandao mzuri wa marafiki ndani na nje ya nchi na kuwa na miradi mbalimbali inayonisaidia kuendesha maisha yangu ya kila siku,” anasema.

WATANZANIA NI WAKATI WA KUOMBA

MAELFU WAJITOKEZA KUFANYA MAOMBI YA TOBA KWA TAIFA JIJINI ARUSHA HII LEO

Maelfu ya wakazi wa jijini Arusha, wamekusanyika siku ya leo katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abed Karume jijini humo kwa ajili ya kufanya maombi ya toba kwa ajili ya taifa, maombi hayo ambayo yameratibiwa na makanisa mbalimbali mkoani humo yamevuta umauti huo ambao umeweka rekodi kwa tukio kama hilo.

Kati ya vitu ambavyo vimeonekana kuwagusa watu wengi ni kitendo cha baadhi yao kuamua kuvaa magunia na kumlilia Mungu ili apate kulisamehe taifa, serikali na watu wake, ambapo licha ya watu hao pia wachungaji kutoka makanisa mbalimbali mkoani hapo wanashiriki maombi hayo ya toba huku jeshi la polisi likiwa limeimarisha ulinzi uwanjani hapo.
















UMOJA WA MAKANISA DAR ES SALAAM KUMLETA DON MOEN.

Umoja wa makanisa ya Dar es salaaam ukishirikiana na shirika la kimataifa la LUISPALAU association,liko kwenye mikakati la kufanya tamasha kubwa la injili la upendo maeneo ya Jangwani kuanzia mwezi wa nane hadi mwezi wa 12 mwaka huu, na tamasha hili litafanyika jijini Dar es salaam kama sehemu ya mfululizo wa matamasha ya jinsi hiyo ambayo shirika hilo imekuwa ikiyaendesha katika miji mikuu kadhaa barani Africa.


Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,iliyoundwa na makanisa mbalimbali jijini hapa,tamasha hilo litawaleta nchini wanamichezo mbalimbali wa kimataifa pamoja na waimbaji mashuhuri wa injili,akiwemo Don Moen,Nicole Mullen na wengine wengi,taarifa hiyo imebainisha kuwa wanamichezo wa kimataifa wanaoruka na pikipiki pamoja na baiskeli ya mashirika ya BMX na Fmx nao pia wataalikwa.
Nicole Mullen.

Kwamujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa tamasha hilo Askofu Philemon Tibanenason ameongeza kuwa makanisa hayo yamepata fursa ya pekee ya kufanya kazi katika umoja kudhihirisha upendo wa Yesu ubadilishao maisha,tamasha hilo limewahi kufanyika katika miji kama Kigali Rwanda,Bujumbura Burundi,Kampala Uganda na Cairo Misri.

KWA TAARIFA YAKO - LICHA YA KUPATA MCHUMBA MALOPE HATAKI NDOA, PIA AFADHILIWA KWA KUPIGWA MAKOFI NA WAIMBAJI WAKE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Rebecca akiwa na mchumba wake bwana Tshabalala walipokuwa kwenye mahojiano WAPO Radio FM.
Leo katika kipengele cha KWA TAARIFA YAKO tunaelekea huko nchini Afrika ya kusini ambako tunakutana na mwanamama malikia wa muziki wa gospel barani Afrika bibie Rebecca Malope mama huyu ambaye ana umri wa miaka 44 sasa ni kwamba kama tulivyowahi kuandika alipotembelea nchini mapema mwaka huu wakati wa pasaka kwamba baada ya kukaa mpweke kwa miaka mingi mwanamama huyu kwasasa amepata mchumba aitwaye Themba Tshabalala.

Mchumba ambaye pia alikuja naye nchini, lakini linapokuja suala la kufunga ndoa mwanamama huyu anasema bado mapema saaana kwani anataka kwanza wafahamiane vyema na mchumba wake huyo ambaye pia ni mmoja wa mameneja wake. Amesema mpaka sasa amewakataa wanaume watatu waliokuwa tayari kumuoa kwasababu hakuwa tayari, ila anadhani mwanaume huyu ndio mwafaka ingawa anasema bado yupo yupo kwanza kwenye suala la kufunga ndoa.

VITUKO VYA WAIMBAJI ALIOWATOA KIMUZIKI

Mwanamama huyu ambaye anamafanikio sana kwenye medani ya muziki barani Afrika, amewatoa waimbaji wengi sana akiwemo Lundi Tyamara mwanakaka ambaye ukisikiliza sauti yake inafanana na Rebecca, pia ni mwimbaji aliyekuwa mwitikiaji katika band ya Malope, lakini cha ajabu ni kwamba kati ya waimbaji wawili waliokuwa wanataka uadui na Rebecca ni mwanakaka huyu na dada mwingine ambaye alidiriki hata kumpiga makofi Rebecca kutokana na kile kwamba mwimbaji huyu anakubalika sana, kufuatia tukio hilo Rebecca alikaa kimya ingawa vyombo vya habari nchini humo viliandika tukio hilo.

Pamoja na hayo Rebecca ameendelea kusimama katika huduma pamoja na mashambulizi na maneno mengi yaliyowahi kusemwa juu yake na waimbaji hao likiwemo suala la mwanamama huyo kuhusishwa na ulevi wa pombe, kilichofanyika kwa sasa waimbaji hao wamejirudi na kumuomba msamaha mwanamama huyo huku Lundi akiwa tayari amejishusha kabisa katika suala la Gospel kutokana na shutuma nyingi juu yake kutoka katika vyombo vya habari.

IRINGA KWA MARA YA KWANZA WAWAKUMBUKA MASHUJAA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine katika bustani ya manispaa ya Iringa wakati wa kumbumbuku ya mashujaa Kimkoa
Hawa ndio mashujaa wetu waliokumbukwa leo Iringa

FAUSTIN MUNISHI (MALEBO) APANIA KUGOMBEA URAISI TANZANIA



''Mimi mchungaji Faustin Munishi. Natamka kwamba Nitagombea Urais Tanzania bila chama cha kisiasa. Nitakuwa Mgombea Huru bila siasa. Nitakapokuwa Rais Nitagawana madaraka na Jeshi, pia wadau wote hasa wapiga kura. Ukiritimba wa CCM kutumia madaraka vibaya utakuwa kwenye kaburi la sahau.

EE MUNGU NISAIDIE NIONGOZE TANZANIA. NIPE HEKIMA NIJUWE JINSI YA KUWAONGOZA WATU WAKO WALIO WENGI TANZANIA. AMEN.”
Kundi la Ambassadors of Christ Choir kutoka kanisa la wasabato Remera jijini Kigali nchini Rwanda, linategemea kuingia nchini Kenya kwa mara nyingine mwaka huu ikiwa ni mwaliko wa kwenda kushiriki kambi za kikristo zinazoandaliwa na kanisa hilo katika nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba kwaya hiyo itakuwa nchini Kenya kuanzia July 26 hadi 30 mwaka huu huko Migori eneo la Awendo. Itakuwa mara ya pili kwa kwaya kwa mwaka huu kufanya huduma nchini Kenya ambapo walikuwa huko mapema mwezi wa tano, kwasasa kwaya hiyo inatamba na album mpya waliyoitoa mapema mwezi uliopita walipotembelea nchini.
Baadhi ya waimbaji wa Ambassadors of Christ wakimsifu Mungu.
Baadhi ya wakaka wa Ambassadors of Christ wakishambulia jukwaa walipotembelea jijini Dar es salaam.
Warren katikati na waimbaji wenzake wa Ambassadors of Christ Rwanda, Warren(mtanzania) amekuwa mmoja wa waimbaji wa kundi hilo kutokana na ukaribu wake na waimbaji wa kundi hilo la Rwanda.picha kwa hisani ya Warren

MWIMBAJI WA KUNDI LA THE VOICE LA JIJINI DAR ES SALAAM APATA AJALI

Mwimbaji wa kundi la The Voice linaloundwa na vijana watano aitwaye Obedi John Mark amepata ajali jana usiku majira ya saa tatu maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa anatumia usafiri wa bajaji. kupitia ukurasa wao wa Facebook kundi hilo limetoa ujumbe huu;-''Mwimbaji mwenzetu Obedi John Mark amepata ajali maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa na usafiri wa bajaji akiwa anaelekea Magomeni...Kwa sasa hali yake si nzuri yuko chini ya uangalizi wa Daktari Mvungi ndani ya Hopitali ya Kinondoni na ameumia sehemu za Kichwa, wapendwa tuzidi kumuombea apone haraka''.


Obedi Mark katika pozi.
Aidha mwana blogger mwingine unlce jimmytemu kupitia blog yake amefanya mazungumzo na mdogo wake Obedi nakueleza kuwa hali yake sio nzuri amepata michubuko kwenye Mikono Miguu na sehemu za uti wa mgongo.Kwa sasa yupo hospital Muhimbili.
Gospel Kitaa inamtakia afya njema Obedi Mungu ahusike katika matibabu yake, tungependa kumuona akijumuika na wenzake katika huduma ya kumwinua Kristo.AMEN
The Voice.

BREAKING NEWS....WALI WA SHEREHE WAUA MMOJA 40 HOI IRINGA

Wahanga wa tukio hilo wakiwa hoi kituo cha afya Ipogolo Iringa
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Ipogolo Dkt mary Makundi
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ibofye wilaya ya Kilolo Godfrey Mtete (kushoto) akiwa na mgonjwa mwingine ktk kituo cha afya Ipogolo walikolazwa kwa kula chakula chenye sumu

MTU mmoja mkazi wa kijiji cha Ibofye wilaya ya Kilolo mkoani Iringa amefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamelazwa katika Hospitali mbali mbali za mkoa wa Iringa kikiwemo kituo cha afya Ipogolo na Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kula wali na kunywa togwa zinazosadikika kuwa na sumu katika shehere ya kutoa mahali .

Wahanga wa tukio hilo ambao wamelazwa katika kituo cha afya cha Ipogolo mjini Iringa waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo kuwa tukio hilo lilitokea juzi jumamosi baada ya mkazi wa kijiji hicho Bw James Ngaile kuandaa chakula na kinywaji hicho aina ya togwa kwa kwa ajili ya sherehe ya kuoza binti yake.

Alisema Yamile Mhehe ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya kuwa utaratibu wa chakula katika sherehe hiyo ilikuwa ni sahani moja kwa watu watatu na kuwa chakula kilichoandaliwa ni wali na ugali huku mboga ikiwa ni maharage na kabichi na baada ya chakula wageni walikuwa wakitumia kinywaji aina ya togwa kwa ajili ya kushushia chakula hicho.

Hata hivyo alisema baada ya kula chakula hicho muda wa saa moja usiku wananchi waliofika katika sherehe hizo walitawanyika kurejea majumbani kwao na kuwaacha walengwa wa sherehe hiyo wakiendelea na mapumziko ya usiku.

Alisema baada ya kufika nyumbani muda wa saa 2 usiku tumbo la kuharisha damu lilianza kumsumbua yeye na mke wake na hivyo kulazimika kukimbia kwa majirani kuomba msaada zaidi na baada ya kufika huku walikuta majirani zao nao wakisumbuliwa kama wao hali iliyowalazimu kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye pia alikuwa hajiwezi kutokana na kukumbwa na tatizo kama hilo.

Hivyo kutokana na hali hiyo kuonekana kuwakumba watu zaidi ya 20 katika kijiji hicho uongozi wa kijiji ulilazimika kukodisha daladala na kuwachukua wagonjwa wote na kuwapeleka kituo cha afya Ihimbo na baadhi yao ambao hali zao zilionekana kuwa mbaya walikimbizwa kituo cha afya Ipogolo na wengine Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Godfrey Mtete alisema kuwa tukio hilo ni la kwanza kutokea katika kijiji hicho na kuwa hadi sasa bado hawajabaini tatizo lilikuwa katika chakula ,mboga ama togwa hiyo kwani alisema mbali ya tatizo hilo kuwakumba watu waliofika katika sherehe hiyo baadhi ya watoto kama watatu wamelazwa patwa na mkasa huo japo hawakula chakula wala kunywa kinywaji katika sherehe hiyo.

Mtete alisema hadi sasa mtu mmoja ambaye yeye alikuwa akimwita mjombe wake aliyemtaja kwa jina la Wagila Nyaupumba amefariki dunia kabla ya kukimbizwa hospital kwa matibabu.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa idadi ya wananchi waliopatwa na tatizo hilo ni 40 na kuwa watu zaidi ya 38 ndio ambao walionekana kuwa mahututi zaidi na kukimbizwa kupatiwa matibabu huku baadhi ya wananchi wameendelea kufikishwa Hospitalin jana baada ya kuonekana kuathirika na chakula hicho.

Alisema hatua ambayo kijiji kimechukua kuhusu chakula hicho ni kuzuia chakula hicho kumwagwa wala kupewa nguruwe ili kiweze kuchunguzwa zaidi .

Aidha alisema mbali ya chakula hicho kuwakumba wageni waliofika katika shughuli hiyo ya kuona binti bado bibi harusi mtarajiwa na bwana harusi pamoja na wazazi wa pande zote mbili pia ni wahanga wa tukio hilo .

Mganga mfadhiwa wa kituo cha afya Ipogolo Dkt Mary Makundi alithibitisha kupokea wagonjwa 9 kati ya 40 katika kituo hicho na kuwataja wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho kuwa ni Rafiki Kabogo, Beth Ngaile, Neema Ngaile, Emelia Mwalafi, Edina Mkemangwa, Costanzia Maliga, Ayubu Kaywanga Godfrey Mtete na Yamile Mhehe.

Huku akidai hali zao zinaendelea vizuri na kuwa wagonjwa wengine walifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa na kituo cha afya Ihimbo kwa matibabu zaidi .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael kamhanda alipoulizwa na mtandao huu kwa njia ya simu jana kuhusu tukio hilo alisema bado halijafika ofisini kwake na kuwa pindi litakapomfikia atalitolea ufafanuzi.

BREAKING NEWS.....AJALI YA BASI LA TONY SLEY YAUA RAIA WAWILI WA ZAMBIA NA MTANZANIA MMOJA IRINGA ,38 WAJERUHIWA

Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali usiku wa leo na kuua watu watatu na kujeruhi 38Majeruhi wa ajali hiyo wakipelekwa wodini katika Hospital ya mkoa wa Iringa
Majeruhi Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
Dereva wa basi hilo akifikishwa Hospital ya mkoa wa Iringa akiwa hoi
Ajali mbaya ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzani huku watu 38 wakijeruhiwa .
Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam leo majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake .
Wakizungumza na mtandao huu wa  majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30) .
Bi Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio .
Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.
Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.
Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi wa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya
Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.
Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa .
Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wote wafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.
Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe

MWANDISHI WAPO RADIO KUAGWA LEO KIJICHI

Mwili wa mtangazaji na muandaaji msaidizi wa Michezo wa WAPO Radio FM, Joseph Pancras Mapunda utaagwa leo nyumbani kwake Mtoni Kijichi - Bujonga kuanzia saa nane mchana, baada ya kufanyika ibada. Ratiba nzima ya shughuli iko kama ifuatavyo.

Saa 5 - 6:00 Mchana   -   Chakula Nyumbani kwa Marehemu
Saa 6 - 7:00 Mchana   -   Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani
Saa 7 - 8:00 Mchana   -   Ibada - nyumbani kwa marehemu
Saa 8 - 9:00 Mchana   -   Kuaga mwili wa marehemu
Saa 9 -10:00 Alasiri -  Safari ya kwenda kuupumzisha mwili (makaburi ya Chang'ombe maduka mawili)
Saa 10 Jioni                -   Ibada - (makaburi ya Chang'ombe maduka mawili) Hapa ndipo itakuwa mwisho wa safari ya mpendwa wetu Joseph Mapunda.

Jinsi ya kufika nyumbani kwa marehemu, panda magari ya Mtoni Kijichi au Mbagala Kuu, shuka kituo cha mwisho (CCM) hapo utatembea kama mita mia moja, kuna kituo kinaitwa Zahanati, hapo kuina transfoma kubwa, utakata kona mkono wa kulia, na hapo utakuwa umefika maeneo ya msibani. (kwa Bujonga)
Joseph Mapunda, pia amekuwa kocha wa timu ya WAPO FC kipindi cha uhai wake.
Kwa wale wanaopenda kushiriki rambirambi, wanaweza kufika WAPO Radio FM na kuonana na Joyce Matthew, ama kwa walio mbali, wanaweza kushiriki kwa kutuma mchango wao kupitia tiGO Pesa na M-Pesa kwa namba 0717-572-066 na 0767-572-066.
Joseph Pancras Mapunda, ama kwa jina la utani 'BABU' kama ambavyo amekuwa akiitwa na wanamichezo wenzake WAPO Radio FM, amefariki siku ya jumamosi katika hospitali ya wilaya ya Temeke alipokuwa amelazwa kuanzia alhamisi usiku. kesho yake ijumaa - alikuwa kwenye matibabu, lakini ilipofika jumamosi, ambapo wafanyakazi wenzake walikwenda kumjulia hali baada yakuwa na kikao, ndipo wakakuta mapazia ya kijani yamezungushiwa kwenye kitanda cha Joseph. Madaktari wanasema, Joseph alikuwa na uvimbe tumboni, ndio uliopelekea kumchukua.
Mshtuko ulikuwa mkubwa, uliojawa na hofu - Joseph Mapunda alikwishatangulia, na kuacha mjane na watoto wawili, ambao bao ni wanafunzi shule ya msingi.
Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog