Gari la Meya likiwa halitamaniki.
Wasamalia
wakimuwahisha Hospital, Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali
eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi
la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa
),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe (wa kwanza kushoto) akiwa na
Mkuu wa wilaya ya Morogoro , Said Amanzi , wakipita eneo ambalo gari la
namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya
Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30
alasiri eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar
na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy
Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya
huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Hili ndilo basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Meya
wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba
tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30,
mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu
Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba
za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe
kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva
Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na
HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa
ajili ya kupatiwa matibabu. ( Picha na John Nditi).
Mwandishi
wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye
kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la
namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya
Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30
alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar
na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy
Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya
huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Na John Nditi, Morogoro
MEYA wa
Halmashauri ya Manispaa Morogoro , Amir Nondo (45), dereva na
waandishi wa habari wawili wamepata ajali baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kugongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH,
aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa na kujeruhiwa sehemu
mbalimbali za miili yao na kulazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro.
Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri ,
eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro-
Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.
Majina ya watu hao wengine waliojeruhiwa na kulaza katika wodi za daraja
la kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa , ni dereva wa gari la
Meya, Mwambala Ally (55) , na waandishi wa habari ambao ni wapigapicha
vituo vya televisheni , Anitha Chali (30) pamoja na Hussein Nuha (28).
Mstahiki meya huyo aliyekuwa kwenye gari ya Halmashauri ya Manispaa
hiyo yenye namba za usajili SM 4151, ikiendeshwa na Mwambala ambamo
pia walikuwemo waandishi wa habari hayo na alikuwa katika msafara wa
ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa huo,Dk Rajab Rutengwe.
Meya Nondo akizungumzia ajali hiyo, akiwa wodini akipatiwa matibabu
,sambamba na majeruhi wengine alisema baada ya kufika eneo la
Mizambarauni, Darajani, lilichomoka pembeni basi la abiria ililokuwa
likitokea Njombe kuelekea Dar es salaam, na kuligonga kwa mbele gari
alilokuwemo.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliwaambia waandishi wa habari wakiwa eneo la
tukio, kuwa chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria mali ya kampuni ya
Happy Africa, kuingilia msafara huo wa mkuu wa mkoa uliokuwa ukielea
mjini baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya maabara na
kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bigwa katika Shule ya Sekondari
Sumaye.
Mkuu wa mkoa kwa takribani wiki mbili amekuwa katika ziara katik
halmashauri saba za mkoa huo kwa ajili ya kukagua shughuli za ujenzi na
umaliziaji wa maabara tatu kwa kila shule ya skondari ya Kata na pia
kutumia fursa hiyo kujitambulisha , kusikiliza kero na kuzipatia
majawabu ya msingi.
Januari 29 na 30 mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro na Shule ya sekondari Sumaye kilikuwa ni kituo chake cha
mwisho katika ziara hiyo na baadaye kufanyika kwa majumuisho ya ziara
hiyo Januari 31, mwaka huu mjini Morogoro.
Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa , viongozi
mbalimbali walifika kuwajulia hali wakati wakiendelea kupatia matubabu
na madaktari mbingwa wa hospitali hiyo, akiwemo Mganga mkuu wa mkoa ,
Godfrey Mtei.
Mstahiki Meya Nondo ameumia sehemu ya kichani na mkononi , wakati na
mpiga picha Anita Chali, ameumia kichwani, huku dereva pamoja na
Hussein wakiumia zaidi kwenye paji la uso na kichwani huku Hussein
akisaidiwa na mashine ya kupumulia (oxygen).
Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa imesema itatoa
taarifa ya ajali hiyo jumamosi ya Januari 31, mwaka huu.