Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji,Sera,Utafiti na Mawasiliano,Abubakar D. Asenga
Nimeona taarifa ya Kaka Zitto kabwe akielezea hoja zake kwa msingi wa kukana kumhujumu Rais Magufuli na kuwa waliotoa taarifa hizo wanatumiwa na mmoja wa Mawaziri ( ) wa Serikali ya awamu ya tano.
Kaka Zitto ameenda mbali zaidi akiandika,namnukuu
“maneno hayo yanaenezwa na watu wanaotumwa na Waziri(anamtaja jina) nina ushahidi usio na mashaka wa waziri( ) kupanga vijana wanaojiita wa UVCCM kufanya Mikutano na waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya hivyo” mwisho wa nukuu.
Mosi, nimpongeze Mh. Zitto Kabwe kukana kwa sauti ya juu kabisa kuwa hampingi Rais Magufuli na anamuunga mkono katika Ujenzi wa Nchi kama alivyofanya kwa Serikali ya awamu ya nne.Kama ni kweli na lipo kwa matendo Ni jambo jema sana kwa maslahi ya nchi yetu ambalo wapinzani wengine wanapaswa kuliiga.
Pili,Nimthibitishie pasi na shaka ndugu Zitto Kabwe kuwa Vijana hao kama alivyosema (wanajiita wa UVCCM) ni wanajiita tu.
Vijana wa CCM kama Jumuiya imara ya Vijana wa Tanzania haiwezi kutumika na kulipwa pesa na mtu ili kutumika kwa maslahi binafsi.
Na kwa kuwa ndugu Zitto amelisema jambo hili kwenye umma na kuwa anao ushahidi wa hao wanaojiita wa UVCCM, tupo tayari kushirikiana nae na ikithibitika kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa Kanuni yetu, vinginevyo tunaona jina la Jumuiya yetu linatumika kama Nyanya kwenye mboga za watu,na hatutakubali hilo.
Tatu. UVCCM inaimani kubwa na Rais Magufuli kuwa hawezi kuwa mtetezi wa Majipu ata kama mwenyejipu kwa madai yako ni rafiki yake, na UVCCM ni kisu cha kumsaidia Rais kutumbua majipu hayo.
Lakini tunajua kuwa Rais Magufuli ni Rais makini katika atua anazochukua pasi na kumuonea mtu, kwa kuwa kutumbuliwa jipu kunamaumivu makali sana yanayoweza kuvumiliwa tu na mwenye jipu, asiekuwa na jipu hawezi kutumbuliwa.
Hivyo kama kweli tuhuma hizo zinazotolewa kwa Waziri huyo zina ukweli na zinahusu rushwa na ufisadi Rais angeshamtumbua waziri ama atakuja kumtumbua tu ikishathibitika, tusiwe na haraka,"haraka haraka haina baraka"
0 comments:
Post a Comment