Baada ya kikao cha muda mfupi kilichofanyika kwenye machinjio ya Vingunguti Waziri Nchemba aliyaongea haya ‘Kwanza kuna mambo kadhaa tumeyaona ambayo TFDA wamefanya kazi nzuri sana nawapongeza sana wamebaini ukosefu wa maji, na pia visu vinavyotumika kuchinjia vinasafishwa mahali ambapo sio salama vinasafishwa bafuni‘>>>Mwigulu Nchemba Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji
‘Sasa tulichokubaliana leo ni kwamba watengeneze baadhi ya sehemu ambazo zinawezekana kwasababu vifaa wanavyo na pili kati ya leo au kesho waweke zile mashine za kuning’inizia ngo’mbe wakati wa kuchuna , na la tatu warekebishe mabomba ya maji hapa machinjioni‘>>>Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba
‘Kadri tunavyotaka nyama iwepo katika mabucha yetu wananchi wapate nyama kwa bei nafuu lakini lazima tuhakikishe hiyo nyama ni salama na imechinjwa katika mazingira safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu, sisi kama wizara ya afya ni wajibu wetu kuhakikisha kanuni za afya na usafi zinazingatiwa’ >>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
”Kwa hiyo nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa nyama itakayokuwa kwenye mabucha itakuwa ni nyama salama lakini tutahakikisha tunaendelea kulinda viwango vya nyama ili wasiweze kupata madhara ya kiafya‘>>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Sehemu ya mabomba ya maji
0 comments:
Post a Comment