Jeshi
la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14
na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya
Wilaya ya Temeke.
Kamanda
wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao,
wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya
jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi
kuendesha msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.
Alisema
vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo Kirakala,
Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo ya Mwananyamala
lakini alikamatwa Temeke.
"Kama
Kamanda Simon Sirro alivyosema kuwa ni lazima wahalifu wadhibitiwe
katika mko huu. Temeke hatuwez kumwangusha, tunatekeleza agizo lake," alisema Kamanda Muroto.
Alisema
vijana hao wanajihusisha na vitendo vya uporaji wa mali mbalimbali
kuanzia mitaani, pia kujeruhi watu hali inayosababisha wakazi wa eneo
husika kuishi kwa hofu.
Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.
Wakati
huohuo, Kamanda Muroto amesema polisi inashikilia mwanamke mmoja
mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Buza baada ya kumkuta na puli 120 za
dawa za kulevya aina ya bangi.
0 comments:
Post a Comment