April 16 2016 Rais John Pombe Magufuli
amefanya uzinduzi wa mradi wa barabara ya juu ‘Flyover’ Dar es salaam,
barabara inayotarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2018.
Lengo likiwa ni kupunguza kero za
usafiri katika jijila Dar es salaam, Barabara ambayo inatengenezwa chini
ya usimamizi wa Serikali ya Japani, Katika uzinduzi huo Rais Magufuli
amesema ‘Kuna watu wakati
tukibuni hili jambo walianza kuleta maneno na kusema ni jambo
lisilowezekana, na sasa kazi imeanza na itawezekana, nataka tuifanye
Tanzania kama Ulaya‘
‘Imefika wakati shughuli
nyingi zinaharibika kwa sababu ya foleni, hata baadhi ya ndoa sasa
zinavunjika kwa sababu watu wanachelewa kurudi majumbani kwao, sasa kwa
huu mradi wa barabara za juu nahakika utatatua matatizo yote‘
‘Niwakumbushetu
ndugu zangu, uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa kuwatumikia
watanzania, tuweke uchama na usiasa pembeni na tusimame kwa pamoja
maendeleo ya watanzania‘
Pia Rais Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makondakatika harakati zake za kuhakikisha Dar es salaam inakuwa safi ‘Nimpongeze
sana mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa project yake
aliyoianzisha katika kuifanya Dar es salaam kuwa safi, niwambeni
tumuunge mkono‘
0 comments:
Post a Comment