Home »
» UKIONA DALILI HIZI TAMBUA WEWE NI MCHEPUKO WAKE
SHARIFA HASSA
1. Huwa haongelei stori tofauti na kufanya mapenzi kwa sababu amekufanya wewe ni chombo chake cha starehe.
2. Hata siku moja hayuko tayari kukualika kwenye mkusanyiko wa familia yake kwa sababu hataki ufahamike katika familia yake.
3. Hapendi umtembelee bila kutoa taarifa kama unaenda na kama
ukienda bila taarifa atakuwa mkali sana kwa sababu anaogopa kufumaniwa.
4.Simu zake muda wote ziko mfukoni na hata zikiwa sehemu
inayoonekana lazima kuwe na michoro au maneno ya siri
(pattern\password).
5. Hapendi mkiwa hadharani muonyeshe kwamba nyie ni wapenzi, anataka mapenzi yenu yawe ya kujificha.
6. Hataki mpige picha ya pamoja na hata mkipiga hataki zisambae sehemu yoyote tofauti na kuwa nazo nyinyi binafsi.
7. Anapigiwa simu za ajabu nikisema za ajabu na maanisha kupigiwa simu usiku na akizipokea anaenda kuongelea pembeni.
8. Hana mpango na wala hapendi muongelee maisha yenu ya mbele yatakuwaje au nini hatma ya mahusiano yenu.
9. Hakuruhusu kuwafahamu marafiki zake hata ukipata fursa hiyo hapendi uwe na mawasiliano na rafiki yake yoyote.
10. Sio mwepesi kwenye masuala ya kutoka matembezi yaani yeye anataka mkutane gesti au nyumbani hapendi muongozane.
0 comments:
Post a Comment