Home »
» JANUARY MAKAMBA: MIFUKO YA PLASTIKI NI MARUFUKU KUTUMIKA NCHINI
SERIKALI imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana
bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini,
Edward Mwalongo (CCM).Mwalongo
alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya
mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.
January alisema sasa wanaendelea
kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba Januari Mosi mwakani
itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
Awali, akijibu swali hilo la nyongeza,
Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali
itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya
plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
“Wadau wote, wazalishaji na viwanda
wanatakiwa kuhakikisha wanazalisha mifuko inayoruhusiwa yenye unene
usiopungua mikroni 50, tutachukua hatua kwa viwanda vitakavyokiuka
ikiwemo kufunga viwanda hivyo,” alisema Mpina.
0 comments:
Post a Comment