Home »
» UPINZANI WAIPA ‘HEKO’ NEC KWA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI
Vyama vya siasa vya upinzani
vimeipongeza tume ya taifa ya uchaguzi kwa hatua yake ya hivi karibuni
ya kutoa vyeti vya shukrani kwa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi
mkuu wa mwaka jana hapa nchini na kuelezea hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa
kuaminiana na vyama vya siasa.
Akiongea na waandishi wa habari katika
ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini DAR ES SALAAM,katibu mkuu wa
chama cha NRA,HASSAN KISABYA ALMAS,amesema,kitendo hicho kinaonesha ni
jinsi gani tume ya taifa ya uchaguzi ilivyobadilika kutoka iilivyokuwa
ikifanya mambo yake zamani ambapo ilionekana kutokujali vyama vya
upinzani.
Amesema wao kama vyama vya upinzani
watajitahidi kushirikiana na tume ya uchaguzi kuimarisha amani iliyopo
nchini baada ya uchaguzi katika maisha ya kawaida ya siasa,kutokana na
tume yenyewe kuonesha ukomavu kwa namna ilivyosimamia suala la amani na
utulivu katika uchaguzi mwaka jana kwa kutopendelea upande wowote.
0 comments:
Post a Comment