Home »
» Rais Magufuli Ampaisha Dr. Ramadhani Dau wa NSSF.....Ammwagia Sifa kwa Kazi Nzuri, Azima Ndoto za Wabaya wake
"Kabla
sijaanza kuhutubia, naomba nimkaribishe mtu muhimu sana aliyefanikisha
ujenzi wa Daraja hili. Dkt Dau tafadhali karibu usalimie kidogo’’.
Ndivyo alivyoanza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli jana wakati wa uzinduzi wa daraja la kihistoria la
kigamboni alilopendekeza liitwe daraja la Nyerere kutukuza mchango wa
mwasisi wa taifa hili baba wa taifa hayati mwalimu Julius kambarage
nyerere.
"Watanzania
wana tabia ya kusahau sana. Tunaweza kuzindua hapa wakashangilia lakini
wasiwapongeze watu waliofanikisha kazi hiyo..mnyonge mnyongeni haki
yake mpeni”. Aliendelea Rais Magufuli mara baada ya Dk. Dau kumaliza kusalimia.
Dk
Magufuli alisema Balozi Dau alimfuata ofisini kwake(wakati huo akiwa
Waziri wa Ujenzi), akiwa mnyonge na mwenye kukata tamaa ya kufanikisha
mradi huo.
“Ndiyo nikamwambia aanze kufanya kazi.” Rais Magufuli alisema
ni Dk Dau na NSSF ndiyo waliosimamia na kuhakikisha daraja hilo
linajengwa na kukamilika kwa kiwango hicho, akasema haitakuwa busara
kulizindua bila kutambua mchango wake.
Alisema ni kawaida kwa watu wenye
michango mikubwa kusahaulika wakati wa mafanikio.
Tukio hilo lilionyesha dhahiri kwamba Rais
Magufuli amevutiwa kwa kiasi kikubwa na
kazi ya mkurugenzi huyo mstaafu wa NSSF na kwenda tofauti na matarajio ya watu
wengi waliokuwa na shauku ya kumsikia Rais akimchukulia hatua mkurugenzi huyo
kwa madai ya ubadhirifu wa mabilioni ya fedha .
Hatua hii ya Rais kumwagia sifa hadharani Dk. Dau, inakuja
siku chache baada ya kusambazwa kwa kinachoitwa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za
serikali CAG taarifa ambazo baadae zilikanushwa na ofisi ya CAG .
Akizungumza katika
hafla hiyo, Dk Dau alizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa NSSF
katika uwekezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Aliwakumbusha
Watanzania kumtanguliza Mungu akisema kukamilika kwa ujenzi wa daraja
hilo kutasaidia kukuza uchumi na kurahisisha usafirishaji kwa wakazi wa
Kigamboni na Tanzania kwa ujumla.
Katika hotuba yake, Rais Magufuli
alisema daraja hilo ni la kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati na kwamba litasaidia kukuza uchumi, utalii na ndiyo maana hata
majirani wanalitamani.
“Daraja hili linabeba zaidi ya tani elfu moja, ni
daraja la kipekee, linao uwezo wa kudumu kwa zaidi ya miaka 100,”
alisema .
Alisema katika ujenzi wake uliofanyika kwa utaratibu wa PPP
(Public Private Partnership), Serikali imetoa asilimia 40 na NSSF
asilimia 60 hivyo vyombo vya usafiri kama baiskeli, guta, pikipiki na
magari yatalipa kuvuka.
“Leo hii, daraja hili limekamilika... halitambagua mtu kwa sababu wa CCM watapita hapa wa Chadema watapita hapa na
bahati nzuri mstahiki meya wa jiji hili ambaye ni Chadema naye yuko hapa
na amepita katika daraja hili… lakini wananchi waenda kwa miguu
hawatalipia matumizi ya daraja… ila wale waendesha baiskeli, pikipiki,
maguta na magari lazima walipie,” alisema Dk Magufuli.
Rais aliipongeza
kampuni ya China Railway Construction Engineering Group iliyotekeleza
mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya China Railway Major Bridge
Group.
0 comments:
Post a Comment