Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia bandari ya Tanga baada ya kuwepo na ushindani na bandari za Lamu na Mombasa
za nchini Kenya. Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima katika Ziwa Albert
nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya
Tanga ambako ndiko meli kubwa za mafuta, zitakapotia nanga kubeba mafuta
hayo kwenda sehemu mbalimbali duniani.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
April 24 2016 amewasili Tanzania akitokea Uganda alipokwenda kwenye
mkutano wa majadiliano ya bomba hilo la mafuta lipite wapi kati ya
Tanzania au Kenya. Akizungumza baada ya kuwasili Prof. Muhongo
ameeleza sababu zilizofanya Bandari ya Tanga kuchaguliwa ambapo
ushindani ulikuwa ni wa ubora wa bandari na ubora wa njia ambako
bomba litapita……….
>>>’Tanga
ni bora kwa sababu ina kina kirefu kulinganisha na bandari za mombasa
na Lamu, Bandari ya Tanga ina kina cha zaidi ya mita 23 ambayo kimataifa
inatakiwa ili meli kubwa inayokuja kuchukua shehena ya mafuta iweze
kutia nanga na kupakia mafuta nakuondoka, tumewapiku wenzetu kwa kina,
na pili bandari yetu inaweza kufanya kazi kwa siku zote za mwaka yaani
siku 365′:-Profesa Sospeter Muhongo
Bomba
hilo litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika
mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya
Tanga. Bomba hilo linatarajiwa kukamilika mwaka 2020 katikati.
0 comments:
Post a Comment