APRIL 29 2015 MAGAZETI ya TANZANIA leo yameandika hizi kubwa >> Udaku,
Posted by Unknown
Posted on 9:06 AM
with No comments
Posted by Unknown
Posted on 8:59 AM
with No comments
MKE ACHINJWA KISA KWENDA SALUNI NA KUPENDEZESHWA, MAJIRANI WADAI ASINGEKUFA MKE ANGEKUFA MUME.. SIMULIZI YAO INASIKITISHA.
Enzi za uhai wake, Mary Lucas (20) anaedaiwa kuchinjwa na mumewe.
Tukio hilo lililoacha
simulizi ya kushangaza miongoni mwa wanandoa na wanaotarajia kuingia,
lilijiri Aprili 18, mwaka huu nyumbani kwa mwanaume huyo, Mtaa wa
Mapinduzi ‘A’ Kata ya Duga jijini hapa.
WANACHOKIJUA POLISI WA TANGA
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Tanga, ACP Zuberi Mwombeki alitangaza kwa waandishi wa habari kwamba,
mauaji hayo yalitokea saa nne na nusu asubuhi ya Aprili 18 mwaka huu.
Alisema chanzo cha tukio
hilo ni wivu wa kimapenzi kati ya wawili hao ambapo marehemu alimuomba
mumewe pesa kiasi cha shilingi elfu kumi aende saluni kutengeneza
nywele lakini mwanaume akasema hana.
“Mwanaume hakumpa pesa
marehemu lakini baadaye alimkuta amesuka na ndipo ugomvi ulipoanzia hapo
hadi kutokea mauaji hayo,” alieleza kamanda huyo.
UWAZI LAANZA NA MAJIRANI
Mengi yamesemwa kufuatia
mauaji hayo, lakini kama kawaida ya Gazeti la Uwazi ni kufuatilia kwa
kina ili kujua chanzo cha kila habari inayotakiwa kuandikwa gazetini.
Ili kujua nini kilitokea
kabla na baada ya mauaji hayo, Uwazi lilizungumza na baadhi ya majirani
wa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi
chini ya ulinzi mkali.
“Jamani sisi wenyewe
tumeshtuka sana kwa kifo cha Mary, mimi nimeongea naye akiwa anakwenda
saluni na hata aliporudi. Kama angejua ndiyo siku yake ya kufa naamini
asingekwenda. Inauma sana!
“Mary alitoka saluni
akiwa amependeza maana alitengenezwa nywele vizuri sana. Mimi mwenyewe
nilimsifia. Kufika nyumbani kwake, mzozo ukaanza.
“Mumewe alitaka kujua
alikotoa shilingi elfu kumi ya kuendea saluni maana yeye hakumpa. Mzozo
ulikwenda hadi mwanaume akachukua panga na kumchinja. Naamini ni wivu,”
alisema jirani mmoja.
KUMBE WALIKUWA NA HISTORIA YA UGOMVI
Jirani mwingine, Shaban
Juma yeye alisema: “Hawa watu wameishi katika hali ya kutoelewana na
walikuwa wakigombana kila wakati, lakini hatukujua kama litatokea hili
kwani mara zote katika kugombana kwao, mwanaume ndiye aliyekuwa akipigwa
jambo ambalo liliwafanya watu wa karibu yake kumshauri kuvunja
uhusiano wao kulikoni aibu ya kupigwa na mke.”
Jennifer Charles yeye
pia ni jirani, alisema: “Siku ya tukio Mary alimwomba mumewe hela ya
kwenda kutengeneza nywele saluni lakini mume hakuwa na pesa siku hiyo
lakini baada ya kuondoka nyumbani, marehemu naye alikwenda saluni.
“Baadaye mume aliporudi
nyumbani hakumkuta Mary lakini mara alirudi akiwa ametengenezwa nywele
jambo lililomfanya bwana kuhisi kuwa fedha hizo amehongwa na mwanaume
mwingine tofauti na yeye na hivyo kuzuka ugomvi huo.”
MUME ALITOKA NJE AKITAMBA KUUA
Baada ya Jennifer
kumaliza kusimulia hayo, Juma Ally, naye ni jirani, akaendeleza:
“Hatukujua kilichoendelea katika mzozo wao, lakini baadaye ukimya
ulitawala. Muda mfupi mbele mume alitoka nje na kutuambia kwamba
ameshaua huko ndani kwani amechoka kupigwa na sasa amejibu mapigo.
“Kwanza tulijua anatutania lakini tulivyoona kimya kimezidi tukaamua kuingia ndipo
tulipomkuta marehemu
akiwa chini, akitoka damu nyingi. Tuliogopa kwa kweli. Mary mrembo
tunayemjua sisi, amelala chini na damu chapachapa.
“Alikuwa ana majeraha
makubwa sehemu ya shingo na kichwani yaliyotokana na kupigwa na panga.
Ilionekana panga lilikuwa kali sana na panga lenyewe lilikuwa pembeni
yake. Ndipo tulipoamua kumkimbiza Hospitali ya Mkoa, Bombo ambapo
alipoteza maisha wakati madaktari wakihangaika kuokoa uhai wake.”
ASINGEKUFA MKE
Naye, Fatuma Ramadhani
alisema kutokana na ugomvi wa mara kwa mara kati ya wawili hao na
mwanaume kupigwa kila wakati, majirani waliamini siku moja mume huyo
ndiye angekuja kupata madhara hata kufa kutokana na alivyokuwa akipigwa.
MTUHUMIWA KUPANDA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE
Kamanda Mwombeki alisema upelelezi unaendelea ili kuweza kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
Marehemu Mary alizikwa katika eneo la Mwakizaro jijini Tanga, siku ya pili baada ya tukio hilo la kuhuzunisha.
Posted by Unknown
Posted on 8:56 AM
with No comments
RAIS KIKWETE AZINDUA MELI MBILI ZA KIVITA ZA KIKOSI CHA WANAMAJI CHA JWTZ JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi meli mbili za doria bahari kuu TNS
Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la
Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita
mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe
zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam
leo April 28, 2015
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli
vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe
zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam
leo April 28, 2015
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la
Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro
Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS
Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la
Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Posted by Unknown
Posted on 7:25 AM
with No comments
Watanzania 26 Waliokuwa Afrika Kusini Warejea Nyumbani.......20 Wengine Kuhakikiwa na Kurejeshwa
Kundi la Watanzania 25 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini jana tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania
hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix
zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi
la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini.
Wakati
huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa
kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough
jijini Johannesburg.
Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
Posted by Unknown
Posted on 7:23 AM
with No comments
Zaidi ya Watu 900 Wadaiwa Kupoteza Maisha kwa Tetemeko la Ardhi Nchini Nepal
TETEMEKO
la ardhi limetokea nchini Nepal jana na na kupoteza
maisha ya watu ya 900 na kuangusha Mnara wa Karne ya 19 Mjini,
Kathmandu pamoja na kusababisha maporomoko ya theluji kutoka katika
milima.
Taarifa
zinadai kuna uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo
lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara mji
wa pili kwa ukubwa nchini Nepal.
Tetetemeko
hilo la ardhi ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi
cha miaka 81 na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani
kaskazini mwa India na Bangladesh.
Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.
Naibu
balozi wa Nepal mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa
mamia ya watu wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa
kila sehemu kubwa na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali
ni nchi nzima imeathirika.
Nepal
ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo
mwaka 1934 likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha
yao.
Baadhi
ya Waokoaji wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo
aliekuwa amefukiwa kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma
kutokana na tetemeoko hilo.
Sehemu ya athari za tetemeko hilo.
Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.
Wananchi wa Nepal wakishirikiana kwa pamoja kuvuta kamba.
Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.
Posted by Unknown
Posted on 7:19 AM
with No comments
Muuguzi amchapa mjamzito viboko......Ni wakati wa uchungu wa kujifungua, Mtoto afia tumboni.
Muuguzi
mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na
kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati
akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto
aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.
Aidha,
mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu
(ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa
kuwa mbaya.
Mwanamke
huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya
wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata
mtoto wake akiwa hai.
Akisimulia
mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka
huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili
za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy.
“Nilishuhudia
Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana
uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia
asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.
Alisema
muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa
akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika,
alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.
“Kesho
yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia
gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali
aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali
ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.
Alisema
Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba
17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika
ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.
“Yaani
ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia
upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni
zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.
Viongozi
wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo
walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata
hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo
kwa mgonjwa huyo.
Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.
Alisema
pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua
zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito
huyo.
“Mimi
sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini
awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji,
nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa
kamili,” alisema.
Afisa
Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada
ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Mdogo
wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa
hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano,
dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili
tu, kwa sababu ya kudeka kwake.