Sentensi 18 za Mbunge Edward Lowassa wakati anatangaza kugombea Urais leo May 30 2015 Arusha
May 30 2015 inakuwa
siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa
Tanzania.. Bado miezi michache ufanyike Uchaguzi Mkuu, mmoja ya watu
ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo vya
habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
katikati ya Jiji la Arusha umeshuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu
ambao walikuja kwa ajili ya kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia rasmi
kabisa kwamba atagombea Urais mwaka huu.
“Watanzania
wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo..
Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya
CCM watayatafuta nje ya CCM. Sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM
tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”>>> Edward Lowassa.
“Nchi yetu
inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa
kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. Aweze kuwaunganisha
Watanzania na kutoa utofauti kati ya walio nacho na wasio nacho“>>> Edward Lowassa.
“Nina hamu, nina shauku na nina uwezo
wa kuiongoza Tanzania… Ninaamini nina kila kigezo cha kuibeba dhamana ya
nchi yetu.. Katika vitu ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita
ya Kagera, nilishiriki kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele
kuikomboa nchi yetu, muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?”
“Kwa wingi
wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kuwa ombaomba… Haya
ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza
nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini..
Uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendeleo”– Edward Lowassa.
“Najua
Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki
zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula
kama wewe“
“Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana“>>> Edward Lowassa.
Sauti yake iko hapa, ukiplay utasikia hotuba yake yote
0 comments:
Post a Comment