KIMENUKA! Ikiwa ni siku
moja tu kabla ya kufungwa kwa ndoa kati ya Zuhura Omari na Abdallah
Salehe, katika hali isiyotarajiwa, mke mtarajiwa amekataa kushiriki
tendo hilo la kheri licha ya taratibu zote kukamilika na kusababisha
tafrani kubwa huko Buguruni Kwa Mnyamani jijini Dar mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Tukio hilo lilitokea Mei
23, mwaka huu wakati ndugu wa mume walipokusanyika nyumbani kwa
Abdallah tayari kwa shughuli, lakini wakalazimika kuondoka baada ya
kuelezwa kuwa mwanamke amekataa kuolewa, ikidaiwa ni mara ya pili baada
ya kufanya hivyo tena mwaka jana.
Shuhuda wa tukio hilo
aliliambia Ijumaa kuwa baada ya kukataa mwaka jana, taratibu nyingine
zote, ikiwa ni pamoja na mahari na zawadi ndogondogo zilipelekwa ukweni
na ndoa hiyo ikapangwa kufungwa Mei 22, mwaka huu, lakini ghafla
wakapata taarifa hizo za kushangaza.
Akizungumza na gazeti
hili, mdogo wa mume mtarajiwa ambaye alipewa jukumu la kumwakilisha kaka
yake kwenda kumchukua mke, aliyefahamika kwa jina la Salehe alisema
hadi siku hiyo, walikuwa wameingia hasara kubwa, hivyo kutaka walipwe
gharama zote walizotoa, ikiwemo mahari (450,000), kitanda, godoro,
kabati na magunia ya mchele uliokuwa upikwe shughulini.
Mmoja wa wanafamilia wa bwana harusi.
Waandishi wetu waliokuwa
eneo la tukio waliwashuhudia baadhi ya mawifi wakiwa katika sare zao za
madela wakingojea muafaka wa harusi hiyo huku wengine wakiandamana hadi
nyumbani kwa bibi harusi wakidai ufafanuzi zaidi.
Bi harusi ambaye aliomba
asipigwe picha alikiri kuwa ni mchumba wa Abdallah kwa mwaka mmoja na
alitakiwa aolewe Mei 23, mwaka huu, lakini aliamua kubadili msimamo
akidai mchumba wake ni mtata kwani amekuwa akimtuhumu kutembea na mpemba
mmoja (jina halikupatikana).
“Huyo Mpemba nilisoma naye sekondari, kwa sasa ni rafiki yangu wa kawaida. Nimegoma kuolewa kwa sababu mwanaume ni mtata sana.
Mmoja wa wanafamilia akiwasiliana kwa simu.
Binafsi nimeshindwa kwa
sababu malengo yangu siyo niolewe leo halafu kesho nirudi nyumbani,
nataka nikae na familia, tuzae tukiwa na amani na mume wangu, ila kwa
huyu nimeshindwa, kama wameandaa pilau lao huko lidode tu,” alisema
Zuhura huku mama yake akidai wamesharudisha baadhi ya vitu walivyopewa.
Jitihada za kuzungumza na bwana harusi hazikuzaa matunda ila jitihada za kumtafuta zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment