Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki WALAANI Jaribio la Mapinduzi Burundi......Aliyetangaza Mapinduzi Asema Kiburi Chake Kimemponza
WAKUU wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamelaani jaribio la mapinduzi ya kumng’oa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na kutaka Katiba ya nchi hiyo ifuatwe ili kudumisha amani na utulivu nchini humo.
Aidha, wameagiza mamlaka husika nchini Burundi kutangaza kusimamisha
kwa muda uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike Juni 26 mwaka huu ili kurejesha
hali ya amani katika nchi hiyo.
Akizungumza jana katika kikao cha ndani kilichofanyika kwa takribani
saa nne kutokana na mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki, Mwenyeikiti wa Mkutano huo, Rais Jakaya Kikwete alisema hatua
ya kufanya jaribio la mapinduzi halitasaidia kuleta amani katika nchi
hiyo.
“Tumekuwa na vikao kwa muda wote tangu asubuhi mpaka muda huu
tukijadili suala la Burundi. Tukiwa tunaendelea na vikao kukawa na mambo
yanaendelea Bujumbura. Kama Jumuiya tunalaani mapinduzi ya Burundi na
jumuiya inaona kuwa hatua hiyo hataisaidia kumaliza hali ya sasa, hivyo
tunataka kuheshimiwa kwa Katiba."
Aliongeza: “Kwa hali iliyopo sasa nchini Burundi, Jumuiya inaona sio
mwafaka kufanyika uchaguzi, hivyo tunaziagiza mamlaka husika nchini
Burundi kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo na ufanyike ndani ya
kipindi cha utawala wa uongozi wa sasa kwa muda usiozidi muda wa utawala
wa sasa.
Aidha, Kikwete alisema jumuiya itaendelea kuzungumza na wadau wote
katika kuhakikisha hali ya amani inarejea ili uchaguzi uweze kufanyika
kwa uhuru na haki kwa kuzingatia katiba ya Burundi, sheria ya uchaguzi
na kuzingatia maazimio ya Arusha.
“Pia tunalaani vurugu zinazoendelea, hivyo tunavitaka vyama vyote
kuhakikisha wanazuia na kuacha vurugu. Jumuiya haitakubali kuona vurugu
zinaendelea,” alisema.
Kikwete alisema wakuu wa nchi ya jumuiya hiyo, watakutana baada ya
wiki mbili kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua stahiki. Hata hivyo,
pamoja na Rais Nkurunziza kuwapo nchini jana, hakuweza kufika katika
ukumbi wa mkutano Ikulu.
Baadaye jioni ilielezwa Rais Nkurunziza anayeiongoza Burundi tangu
Agosti 26, 2005 aliondoka kurejea nchini mwake, lakini habari ambazo
zimetufikia asubuhi hii zinasema rais huyo alishindwa
kutua jijini Bujumbura, Burundi na hivyo kurejea tena jijini Dar es
Salaam.
Katika mkutano huo, mawaziri wa mambo ya nje na Katibu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera walikuwa wa kwanza kuingia katika
mkutano huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliingia ukumbini hapo majira ya saa 7.00 mchana ambako
alifanya kikao cha ndani na mawaziri wa mambo ya nje wa EAC kwa saa moja
kabla ya kuanza kuingia wakuu wa nchi za jumuiya hiyo.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliwasili ukumbuni hapo saa 8:12 mchana
na kufuatiwa na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, na
baadaye Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
ambao walifanya mkutano wa ndani kupitia na kujadili ripoti ya timu ya
mawaziri wa mambo ya nje.
Wengine waliokuwamo kwenye kikao hicho, mbali ya Ramaphosa
aliyemwakilisha Rais Jacob Zuma, mpatanishi wa mgogoro wa Burundi
aliyeachiwa jukumu hilo na aliyekuwa Rais wa Kwanza, Nelson Mandela
ambaye naye aliachwa jukumu hilo na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere, pia alikuwepo Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU)
na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola ambao ni mwenyekiti Maziwa Makuu.
Hata hivyo, hali ya hewa ilibadilika ukumbini hapo kwa waandishi wa
habari na wajumbe mbalimbali wakiwamo wawakilishi wa mataifa mbalimbali
baada ya kutokea taarifa za kufanyika mapinduzi nchini Burundi huku
mkutano ukiwa unaendelea.
Hata Rais Kikwete ambaye alitoka nje ya mkutano kwa dakika kadhaa
hakuwa katika hali ya kawaida na kukataa kuzungumza chochote baada ya
waandishi wa habari kumtaka kuzungumzia kinachoendelea.
Machafuko Burundi
Wakati mawaziri na marais hao wa EAC wakiendelea na kikao jijini Dar es Salaam, vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti juu ya tukio la kupinduliwa kwa Nkurunziza ikielezwa kwa sasa jeshi limeitwaa nchi hiyo.
Wakati mawaziri na marais hao wa EAC wakiendelea na kikao jijini Dar es Salaam, vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti juu ya tukio la kupinduliwa kwa Nkurunziza ikielezwa kwa sasa jeshi limeitwaa nchi hiyo.
Mkuu wa Majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Godefroid Niyombareh
alikaririwa akisema maofisa waandamizi nchini humo wamemkana Nkurunziza
kutokana na machafuko yaliyoibuka hivi karibuni baada ya kiongozi huyo
kutangaza kuwania urais katika kipindi cha tatu mwezi ujao.
Alitangaza kuwa hadi sasa Kamati ya Ukombozi ya Taifa imeundwa kwa
ajili ya kuiongoza kwa muda nchi hiyo.
Jenerali Noyombareh, alisema hatambui uongozi wa Nkurunziza kwa kuwa kitendo chake cha kuwania kipindi cha tatu cha urais ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo.
Jenerali Noyombareh, alisema hatambui uongozi wa Nkurunziza kwa kuwa kitendo chake cha kuwania kipindi cha tatu cha urais ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo.
Tangu jana mchana vikosi mbalimbali vya jeshi nchini humo
vilitawanywa sehemu mbalimbali za Burundi, ikiwemo ofisi za mashirika ya
Utangazaji ya Taifa hilo.
Katika ukurasa wa Twitter wa Rais Nkurunziza, umeandikwa kuwa jaribio la kupindua nchi hiyo la majenerali wa juu wa nchi limeshindikana.
Katika ukurasa wa Twitter wa Rais Nkurunziza, umeandikwa kuwa jaribio la kupindua nchi hiyo la majenerali wa juu wa nchi limeshindikana.
Machafuko yalianza nchini humo tangu Aprili 26, mwaka huu na
kusababisha zaidi ya vifo 20. Aidha pamoja na taarifa hiyo ya Niyombare,
vyombo vingi vya habari vya kimataifa vimebainisha kuwa bado
havijathibitisha mapinduzi hayo.
Maelfu ya wananchi wa Burundi wanaokadiriwa kufikia 50,000 wamekimbia nchi hiyo kwenda nchi jirani kuepuka machafuko hayo.
Tanzania pekee inakadiriwa kupokea zaidi ya wakimbizi 20,000
walioingia kupitia mipaka ya Kagunga wilayani Kigoma Vijijini, mkoani
Kigoma na wengine Ngara, mkoani Kagera.
Niyombare, ambaye awali alifukuzwa kazi na kuvuliwa cheo cha Ukuu wa
Usalama, alitangaza kuondolewa madarakani kwa Nkurunziza katika kambi ya
jeshi huku akiwa amezungukwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa jeshi
na Polisi.
“Kutokana na kiburi na kutotii kwake matakwa ya jamii yake na yale ya
kimataifa yanayomtaka aheshimu Katiba na Makubaliano ya Amani ya
Arusha, Kamati ya Mapatano ya kitaifa, imeamua kumuondoa madarakani Rais
Nkurunziza na Serikali yake,” alisema.
0 comments:
Post a Comment