Huyu Ndo Zitto Kabwe Ninayemfahamu Ambaye CHADEMA Wameamua Kumpaka Matope.
Sijawahi kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo na sijafikiria kujiunga na chama hicho. Nilishawahi kuwa Mwanachama mtiifu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)
Nikiwa
ndani ya CHADEMA nimewahi shiriki katika harakati nyingi zote
zikiwa na lengo la kukikuza chama ambacho niliamini ndo
mkombozi wa kweli wa mtanzania.
Bahati mbaya sikuwa sahihi, nilikosea kukiamini chama hicho ambacho idadi kubwa ya viongozi wake ni mahafidhina.
Nikiwa
ndani ya siasa, nimefanikiwa kujuana na wanasiasa wengi wakubwa
kwa wadogo, mmoja wao ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto
Kabwe.
Namjua
Zitto, nafahamiana naye vizuri, ni mmoja wa wanasiasa wasomi,
wenye siasa safi ambaye mara zote kauli na hoja zake zimetaliwa
na busara na nia ya kulijenga taifa, siwezi kusema si
mbinafsi moja kwa moja lakini nina imani nae kubwa kuwa si
mbinafsi.
Zitto
ameweza kuzimudu siasa safi za taka zilizokuwa zikiendeshwa
ndani na nje ya chadema kabla ya kuhamia ACT- Wazalendo.Ameweza
kupambana na kupenya kwenye changamoto nyingi za kisiasa hasa
siasa hizi za kuwa na chama kimoja kikongwe na chenye nguvu
nchini na nje ya nchi.
Sote
tunaijua CCM ni chama chenye wanachama na viongozi wanaoijua
siasa, wanaweza kukibadili chama hicho wakati wowote, chama hiki
kikuu nchini ni kama kinyonga, kinabadiilika kulingana na
mazingira na wakati.
CCM
kinapanga vyema karata zake, kina propaganda zenye kuwiana na
ukweli tofauti na ilivyo kwa upinzani ambao wanadanganya
wananchi mpaka wanajidanganya wao wenyewe.
Zitto
ameweza kupenya kote huku na ndio maana leo hii, Zitto
anaposulubiwa hata CCM kinaumia na kumhurumia, kwa sababu
wanamjua mwanasiasa huyu kijana ni mtu wa namna gani.
0 comments:
Post a Comment