Mnamo 13 mwezi May jenerali
mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi
amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa
rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidiz mdogo katika
jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini
Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa
kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
16.10-RNTB yarudisha matangazo
Kituo cha redio cha Burundi RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa kimeanza kurusha tena matangazo.
15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusamehe
Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.
15.47pm-Ramani ya Burundi
Ramani ya taifa la Burundi.
15.45pm-Mji wa Bujumbura
Mji wa Burundi Bujumbura ulivyo kwa sasa
15.30pm-Vyombo vya habari vyazimwa
0 comments:
Post a Comment