..!! WANANCHI WALIOKUBWA NA MAAFA YA MVUA YA MAWE KAHAMA, WAFUNGA BARABARA YA KAHAMA KWENDA MIKOANI HADI SERIKALI IWAGAWIE MISAADA
Jinsi Magari yalivyozuiwa katika eneo hilo.
Abiria wanaokwenda mikoa
ya Mwanza, Singida na Dar es salaam na Kwinginenko na wale wanaokwenda
mikoa ya Kigoma na magari yote yanayokwena nchi jirani za Rwanda,
Burundi, Uganda na Congo, wamekwama baada ya Wananchi wa kijiji cha
Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama kufunga barabara kuu ya kwenda
maeneo hayo Aubuhi hii.
Taarifa kutoka eneo la
Tukio zinasema wahanga hao wa janga la mvua ya mawe iliyouwa watu 46 na
kujeruhi wengine zaidi ya 90, wameifunga barabara hiyo kuishinikiza
serikali kuwapa misaada ya chakula na malazi, misaada ambayo imetolewa
katika maeneo mbalimbali huku serikali ya eneo hilo ikiwa haijagawanya
kwa wahanga husika.
Mpaka sasa tayari
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya kahama ambaye pia
ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya ameshaenda eneo la tukio ili
kuwasikiliza wananchi hao na kujaribu kumaliza tatizo hilo.
Hata hivyo taari
tulizozipata hivi punde zinasema kuwa Tayari jeshi la polisi wilaya ya
Kahama limefika katika eneo la tukio na kutumia mabomu ya machozi bila
kuathiri wananchi na kufanikiwa kuwatawanya na kufungua barabara ambapo
tayari magari yameanza kupita.
Ikumbukwe kuwa juzi
Ahamisi Waziri mkuu Mizengo Pinda alikwenda kuzuru eneo hilo lililokubwa
na maafa hayo kwa ajili ya kutolewa kwa misaada ya kibinaadam, ambapo
pia mazao shambani na vyakula vilivyokuwa majumbani pamoja na mifugo
vimeathiriwa.
0 comments:
Post a Comment