MAAJABU YA PETE YA KUOKOTA YALIYOMKUTA HUYU JAMAA… AISEE INAWEZEKANA HATA AKAKATWA KIDOLE
Kijana
mmoja nchini Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete
aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeshaanza
kupuputika huku nyama zikianza kuliwa kimaajabu na kuanza kumtia hofu
kijana huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kama Eric Buageng, alisema
iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani
akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole cha shahada mkono wa kulia,
lakini cha kushangaza baada ya kufika nyumbani alianza kusikia maumivu
kutokana na pete hiyo kumbana kidole.
Eric amesema
kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa
ukitetemeka na alipojaribu kuitupa hakuweza na kusikia sauti ambayo
hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa
lakini hakuweza na kuna wakati anakisikia sauti ikumuamuru atoke nje
lakini haoni mtu yeyote.
Tangu wakati huo jitihada za kujaribu kuitoa pete hiyo zimeshindikana
pamoja na kwenda kwenye Hospitali mbalimbali ikiwemo ya wataalam wa
Jeshi ya 37’ Military na ile ya Korle Bu Teaching bila mafanikio, katika
jitohada za kuhakikisha inatoka alikutana na wachungaji mbalimbali
waliomuombea lakini hakufanikiwa kuitoa.
0 comments:
Post a Comment