Mtoto anadaiwa kuwa ni Nabii, anawatuhumu watu kuwa wachawi.
Hii
inatoka Mbezi Dar, kwenye Hekaheka ya leo msichana anayeishi na wazazi
wake akapata ujauzito lakini alipojifungua akajifungua chatu baadaye
chatu huyo akabadilika na kuwa binadamu wa kawaida.
Mama mmoja anatuhumiwa kuwa mchawi,
amesema alipata taarifa kuwa mtoto huyo ambaye kwa sasa wanamuita nabii
alipandisha mashetani na kumtaja mama huyo kwamba ni mchawi, huwa
anamchukua na kumpeleka makaburini, baada ya tuhuma nyingi kuenea kuhusu
yeye kuna siku watu walitaka kumuua, akaona aende Kanisani kumuelezea
Paroko juu ya matukio hayo.
Mama mmoja muuza samaki amesema kuwa
mtoto huyo nabii alimtuhumu kuwa mchawi na kuwaambia watu kuwa biashara
za samaki na dagaa anazofanya sio samaki ila ni sehemu za siri za watoto
wadogo, kitu kilichofanya biashara yake kuwa ngumu.
Kijana mmoja amesema watu hao ni
matapeli wanaokosanisha watu na huyo mtoto ambaye wanadai ni nabii
aliyezaliwa chatu sio kweli ingawa walimuona msichana huyo wakati akiwa
mjamzito, waliwahi kutoa taarifa katika Ofisi za Serikali za mtaa
wakakaa kikao lakini muafaka haukupatikana.
0 comments:
Post a Comment