MUME WA MTU AMCHOMA KISU HAWARA, NAYE AJICHOMA HADI UTUMBO WAMWAGIKA
Habari zilizolitikisa Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
ni pamoja na ile ya mkazi wa Chamazi, Hussein Mfaume, kumchoma visu
hawara yake, Ester Thomas Ungele (30), naye kujichoma mpaka kujitoa
utumbo, Uwazi limeichimba kwa kina.
Habari zilidai kuwa, kisa hasa cha mwanaume huyo kujichukulia uamuzi huo
wa kikatili ni madai ya mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ni dereva wa teksi.
MANENO YA SHUHUDA MKUU
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mtoto wa Ester, Sarah siku hiyo, yeye na mama yake walikuwa kwenye eneo lao la biashara ya Mama Lishe, nje ya Ukumbi wa Vijana, Amana uliopo Ilala, Dar.

“Ghafla nilimwona Hussein akija huku usoni akionekana mtu mwenye hasira.
Alimfuata mama alipokuwa na kumuuliza ni kwa nini anamfanyia dharau?”
MALUMBANO YAANZA, WAKIMBIZANA
Sarah anaendelea: “Niliona kama malumbano ya kawaida nikawa nawaangalia lakini nikashangaa kumuona Hussein akimsogelea mama na kutoa kisu.“Mama alianza kukimbia naye Hussein akamkimbiza huku bado ameshika kisu mkononi. Niliogopa sana, nikatetemeka. Nilipiga mayowe kumuombea msaada mama.

“Mama alikimbia uelekeo wa kuingia kwenye Ukumbi wa Vijana lakini kabla
hajafika, Hussein alimchota mtama mama akaanguka. Ndipo Hussein
alipoanza kumchoma visu mama sehemu mbalimbali za mwili na kisha kumkita
nacho kichwani.”
KISU MWILINI MWAKE
Sarah tena: “Baada ya kumchoma mama visu hivyo, nilishangaa kumuona Hussein na yeye akijichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake lakini mwisho alijikita nacho tumboni na kuanza kukitikisa kama vile alikuwa anauchanachana utumbo wake, akaishiwa nguvu na kuanguka. Ndipo wasamaria wema wakaanza kuwasogelea.”

Sarah alisema hata yeye alisogea eneo hilo na kuwakuta wote wamepoteza
fahamu huku utumbo wa mwanume ukiwa nje na damu chapachapa ikiwa
imetapakaa mwilini. Wakachukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa
Ilala, Amana, Dar ambapo ni mita chache tu kutoka eneo la tukio.
MKE WA HUSSEIN SASA
Naye mke wa mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zubeda Abeid alipopata nafasi ya kuzungumza na Uwazi alikuwa na ya kusema:“Ukweli taarifa hizi nimezipata kwa mshtuko mkubwa sana hali iliyonifanya nipoteze fahamu. Hussein ni mume wangu wa ndoa, alinioa mwaka 1997 kijijini kwetu, Likombora mkoani Lindi. Tuna watoto wanne.

”Mwaka 2003 tulihamia hapa Dar kutafuta maisha zaidi ya Lindi, mwenzangu
kazi yake ikiwa ni kuuza kahawa pale karibu na huyo hawara yake
aliyemchoma visu. Mimi ni mama wa nyumbani tu.
“Sijui walihitilafiana kitu gani na huyo hawara yake maana leo ndiyo nimejua kumbe mume wangu alikuwa na hawara. Lakini hebu soma meseji hii kwenye simu yangu, alinitumia mume wangu mwanzoni mwa mwezi huu (Februari) bila kuhofia kuwa mimi ni mke wake.”

ILIVYOSOMEKA MESEJI
“MAMA NEEMA NAKUOMBA MESEJI HIYO ISOME PEKE YAKO NA USIMWAMBIE MTU YEYOTE. MIMI NAJIUA KWA SABABU ESTER HANITAKI. WEWE BAKI NA WATOTO, NIMEVUMILIA KUKUFICHA NIMESHINDWA. KWA HIYO MIMI NAJINYONGA, WEWE BAKI NA WATOTO.”

Baada ya Uwazi kuzungumza na mwanamke huyo, lilibahatika kuzungumza na
dalali mmoja wa magari anayefanyia shughuli zake eneo hilo lakini
aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
“Hussein alikuwa akimtuhumu dereva taksi mmoja kwamba anaingilia penzi lake na mwanamke huyo aliyemjeruhi na amekuwa akiahidi kulipa kisasi.

“Yaani leo kama jamaa angekuwepo hapa basi ndiye angekuwa wa kwanza
kuchomwa visu, pengine huyu mwanamke angefuatia,” alisema dalali huyo
aliyeshuhudia tukio hilo.
MGANGA MKUU
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Shaany Mwaruka alikiri kuwapokea majeruhi hao na kusema: “Kwa sasa hali za majeruhi zinaendelea vizuri ingawa awali hali ilikuwa mbaya na kusababisha wakimbizwe chumba cha upasuaji kutokana na kisu kilichotumika kuingia sana ndani ya miili.”

0 comments:
Post a Comment