Baamedi 700 Watunukiwa Vyeti Vya Kimataifa.
Kampuni ya bia ya Serengeti imewatunuku vyeti wahudumu wa baa 700, walioshiriki mafunzo ya kimataifa ya Diageo Master Academy (MBA), yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wahudumu hao ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi.
Akitunuku
vyeti hivyo kwa wahitimu hao jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko
wa Vinywaji Vikali, Stanley Samtu, alisema mafunzo hayo yatawawezesha
wahitimu hao kushiriki shindano la kitaifa na la kimataifa la Diaego
Master Bar Academy.
“Tumewatunuku vyeti vya kimataifa vya MBA wahudumu wa baa kutoka mikoa kumi nchini baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja,” alisema.
Alisema
mafunzo hayo yamewapatia ujuzi wa kuhudumia wateja, kuchanganya bia,
kujua wajibu wao na aina ya vinywaji vikiwemo vya Barleys, Gordons,
Grants, John Walker, Guiness, Smirnoff na jamii zote za bia za
Serengeti.
Alisema
mafunzo hayo ya kimataifa kwa Afrika, yalianza kutolewa Februari 7,
mwaka huu na kukamilika Machi 7 na yaliyolewa na wakufunzi kutoka
Afrika Kusini.
“Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro na Mbeya,” alisema.
Kuanzia
sasa wahitimu wote wameandikishwa katika shindano la kimataifa la
Diageo Master Bar Academy na watahitajika kujibu maswali kwa njia ya
simu ya mkononi.
Alisema
shindano la kuwapata washindi kumi wa juu (top ten), litafanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Aprili 2015 na kila mmoja atapatiwa
zawadi ya dola 1,000 (Sh milioni 1.7) za Marekani.
Alifafanua
kuwa mshindi wa jumla, atapata tiketi ya kushiriki shindano la
kimataifa la ‘Diageo World Class’ litakalofanyika mwaka huu
Johannesburg, Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment