WAUMINI WA KANISA WAKATWA SEHEMU ZAO ZA SIRI ILI WAMUONE MUNGU
Do you like this story?
Ishu ya imani
ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa
mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia
kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.
Sasa hii ya
leo inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni
hamsini duniani Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha
majeruhi kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake 400 kukata sehemu zao za siri
ili waweze kuwa karibu na Mungu.
Wafuasi wa
Singh walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye anaimiliki
ambapo kwenye headlines nyingine mhubiri huyu amekuwa akihusishwa na mauaji ya
mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa
kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa.
Mmoja wa
wafuasi wake, Hans Raj Chauhan aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za
siri kwa sababu alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza
utaratibu huo ulioanzishwa Singh.
0 comments:
Post a Comment