HII NDIO FILAMU YA KUSISIMUA KUHUSU MAUAJI YA ALBINO "FIRIGISI" NCHINI TANZANIA, SASA IKO JIKONI
Picha behind the Scene katika filamu ya "Firigisi" inayohusu ukatili dhidi ya watu wenye albinism. |
Madini yanayotajwa kuwa na uhusiano na vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi
Picha behind the Scene Filamu hiyo
Picha Behind the Scene |
Filamu
ya kusisimua inayohusu ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)
inatarajia kuzinduliwa mwezi April Mwaka huu.Filamu hiyo iliyopewa jina
la “FIRIGISI” imefanywa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga( Bongo Movie
Shinyanga) na msanii Denice Sweya maarufu Dino kutoka Bongo Movie Dar
es salaam.
Dino
ameigiza na kuongoza Filamu hiyo ambayo imebeba maudhui kuhusu Ukatili
wanaofanyiwa watu wenye Albinism nchini Tanzania huku watu mbalimbali
wakitajwa kuhusika katika ukatili huo wakiwemo
wafanyabiashara,wachimbaji wa madini na wanasiasa.
Akizungumza
na Malunde1 blog mjini Shinyanga Mwongozaji wa Filamu hiyo Denice
Sweya( Dino) amesema filamu hiyo ina maudhui mazuri kwani hata mazingira
yake ni ya Kanda ya Ziwa ambako ndiko vitendo hivyo vya ukatili
vimekuwa vikifanyika.
“Ni
filamu ya kiwango cha juu sana inasisimua,imeandaliwa na wasanii kutoka
mkoa wa Shinyanga,msanii pekee kutoka Dar es salaam ni mimi ambaye
nimeigiza na Kuongoza Filamu hii,production yake pia imefanyika Dar es
saalam kwani wapiga picha wanatoka Dar es salaam ambao ni Amani Masuka
akishirikiana na Benny Luoga”,ameeleza Dino.
“Filamu
hii ina maudhui yanayogusa Kanda ya Ziwa kwani ndiyo inaonekana kuwa
ina matatizo makubwa ya ukatili wa watu wenye albinism,tumejitahidi
kuielimisha jamii,tumeonesha,chanzo cha vitendo hivyo, kipi wanapaswa
wajue,nini kifanyike,nini kinawaponza na mambo kadha wa kadha”,ameongeza
Dino.
Dino
amesema washiriki katika filamu hiyo ni watu wanayoyajua vyema
mazingira ya Kanda ya ziwa na kwamba miongoni mwa wahusika wakuu yumo
kijana mwenye Albinism hali ambayo imefanya filamu hiyo iwe katika
kiwango cha juu na wanategemea filamu hiyo itakuwa katika kiwango cha
Kimataifa kwani haijawahi kutokea.
Amesema
mdhamini mkuu aliyetoa mamilioni ya fedha kufanikisha kutengenezwa
kwa katika filamu hiyo ni ndugu Wille Mzava wa mjini Shinyanga na
kwamba filamu hiyo inatarajia kuzinduliwa mjini Shinyanga kati ya Mwezi
Aprili na Mei mwaka huu huku wageni wakiwemo wafanyabiashara
wakitarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi atakuwa mtu
mkubwa sana hapa nchini ingawa hakutaka kutaja jina lake.
Aidha Dino amesema kauli mbiu waliyotumia katika filamu hiyo ni “Albino ni Mimi na Wewe,Tuwalinde,Tuwapende na Tuwathamini(TTT)”
ikiwa ina maanisha kuwa kibaiolojia mwanamme na mwanamke mweusi
wanaweza kukutana na kuzaa mtoto mwenye Albinism,na kwamba ni ndugu zetu
Tunazaa wenyewe kwani huwezi jua kesho kitatokea nini,mtu yeyote
anaweza kuzaa mtoto mwenye albinism.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahim Songoro (Songoro Gaddafi)
amewaomba wakazi wa Shinyanga,kanda ya ziwa na nchi kwa ujumla kuunga
mkono kazi yao ya kwanza na kuahidi filamu hiyo kuzinduliwa haraka
iwezekavyo.
“Hii
ni filamu ya aina yake,haijawahi kufanywa popote duniani,hatujaiga
mahali popote kama wanavyofanya baadhi ya wasanii,na filamu hii inamvuto,inasikitisha,inasisimua,inafunza,inaonya,inaelimisha
kwa kila mtu atakayeiangalia hivyo tunaamini itapokelewa siyo tu
kitaifa bali kimataifa”amesema Songoro
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 comments:
Post a Comment