MVUA YA MAWE ILIYONYESHA SHINYANGA NA KUUA WATU 46 NI “TONADO”: YASEMA MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Agnes Kijazi amesema mvua iliyonyesha Shinyanga na kusababisha maafa kwa jina la kitaalamu inajulikana kama ‘Tonado’, ni mara ya kwanza kutokea hapa nchini.
Kijazi alisema katika ofisi za mamlaka hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Wabunge ya Miundombinu, jijini Dar es Salaam.
Alisema utabiri waliokuwa wameutoa wa saa 24 ulionesha kutakuwa na
mawingu mazito katika eneo hilo, lakini hawakutarajia tonado kunyesha
kwa kuwa sio mfumo wa
kawaida kwa hapa nchini.
Kijazi alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi kumekuwa kukiongezeka
matukio ya hali mbaya ya hewa hata ambayo awali yalikuwa hayatokei.
Alisema tonado, kitaalamu ni mawingu mazito yenye unyevunyevu yanapozidi
uzito yanaanguka mabarafu, hivyo kutokana na mabadiliko hayo upepo
mkali unaozunguka sio hali ya kawaida katika maeneo ya tropiki.
0 comments:
Post a Comment