|
Paul Mwai mwandaaji wa tamasha hilo. |
Wapenzi wa muziki wa gospel jijini Nairobi nchini Kenya wanatarajiwa
kukutanishwa pamoja siku ya tarehe 2 mwezi ujao katika uwanja wa mpira
wa Thika kwenye tamasha kubwa la muziki wa injili lililoandaliwa na
mwimbaji aliyejipatia umaarufu siku za karibuni Paul Mwai ambaye ameamua
kulipa jina tamasha hilo kama Groove awards skiza tune of the year
celebration.
Mwimbaji huyo ambaye amefahamika zaidi nchini kwa album yake ya Racing
Up amewaalika waimbaji mbalimbali kutoka nchini humo akiwemo Emmy
Kosgei, Mbuvi, Pastor Ruth Wamuyu, Ben Githae, Loise Kim, Carol Wanjiru,
Charles Kingori, James Warachi, Muigai Wanjoroge na waimbaji wengine
wengi huku waendesha tamasha hilo ama MC bwana Mwai amewataja kuwa ni
Muthee Kiengei akisaidiwa Olo Matope wa Coro Fm.
Tanzania imekuwa ikisifika katika nyanja ya muziki kwa ujumla nchi za
Afrika ya mashariki ikifuatia Kenya lakini pia katika uchunguzi
uliofanywa na GK kwakusikiliza maoni ya watu mbalimbali inaonekana
kwamba licha ya Tanzania kuwa juu, lakini waimbaji wa nchini Kenya
wameonekana kufanya kazi zao katika viwango vya juu katika recording
audio pamoja na video hali ambayo ni tofauti na waimbaji waliowengi
nchini ambao linapokuja suala la ubunifu katika kazi zao haswa video
mara nyingi muongozo(script) unakuwa mbaya.
|
Paul Mwai katika moja ya huduma zake za kumwinua Mungu. |
|
Emmy Kosgei kuongeza nguvu katika tamasha hilo. |
0 comments:
Post a Comment