mwimbaji wa mahiri wa nyimbo za injili NESTER SANGA KUZINDUA ALBAM YAKE MPYA IITWAYO TWENDENI.
Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za injili Tanzania kutoka Dar el Salaam Nester Sanga ameweka wazi malengo ya uzinduzi wa albam yake mpya jijini Mwanza iitwayo Twendeni ambayo ina takribani nyimbo tisa na imetoka mwezi huu wa nane.Akiongea na mwandishi wa habari hizi bi. Sanga amesema kuwa amefikia uamuzi huu baada ya kupata simu nyingi kutoka Mwanza watu wakimuomba aje afanye tamasha la uzinduzi wa albam yake mpya iitwayo Twendeni.
Akizungumzia ubora wa albam hii ya Twendeni bi. Sanga amesema ni moja kati ya albam ambayo imetokea kupendwa wa watu wa dini na rika zote na kutibithisha kuwa itafanya vizuri kuliko albam yake ya kwanza iliyojulikana ka Jiandaeni.
Uzinduzi wa albam ya Twendeni yake Nester Sanga unatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa kumi katika uwanja wa furahisha Mwanza.
Hii ni albam ya pili yake Mtumishi Nester Sanga ambayo ameitoa baada ya kufanya vizuri na albamu yake ya kwanza iliyojulikana kama Jiandaeni.
Nester Sanga ameanza kuimba siku nyingi baada ya kugundua kuwa ana wito na kipaji hivyo anahitaji sapoti ya watanzania ili waeze kufikia malengo ambayo Mungu ameyaweka mbele yake. Watanzania Tumuunge mkono.
Nester Sanga akiongea na mtandao huu kuelezea kusudi la uzinduzi wa albam yake mpya. |
0 comments:
Post a Comment