SHAMBULIZI KANISANI LAUA WATU 15
Moja ya matukio yaliyopoteza maisha ya watu nchini Nigeria, picha kwa hisani ya nahar.net |
"nathibitisha watu kumi na watano wamefariki" alinukuliwa akisema msemaji wa gavana wa jimbo la Kogi , Jacob Edi. Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo hadi sasa ,lakini kundi la kiislam la Boko Haram limekuwa likilenga makanisa kaskazini mwa Nigeria na pia maeneo ya kati mwa nchi. Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC nchini humo mashambulizi yalifanyika eneo mbali la kusini mwa Nchi ambako kundi la Boko Haram halijavami. Kamanda wa jeshi la muungano katika jimbo la Kogi kanali Gabriel Olorunyomi, alisema kuwa kasisi wa kanisa hilo ni miongoni mwa watu waliouawa.
Waumini wengine wengi walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo na kupelekwa katika hospitali mbali mbali kwa mujibu wa kanali Gabriel Olorunyomi. Maafisa wa utawala wa jimbo hilo, walikuwa wangali wanawatafuta manusura wengine waliokimbilia usalama wao kwenye msitu uliokuwa karibu na kanisa hilo.
Silaha zilizonaswa na maafisa wa usalama Nigeria Mwezi Aprili mwaka huu, maafisa wa ulinzi wa Nigeria walivamia mojawapo ya vituo vilivyoshukiwa kuwa kiwanda cha kutengeza mabomu mjini Okene na kuwaua takriban watu tisa walioshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram.
Mwezi Februari, kundi la Boko Haram lilidai kushambulia jela moja katika jimbo la Kogi kwa kutumia mabomu na zana nzito za vita na kisha kuwaachilia huru wafungwa 119. Hata hivyo mashambulizi mengi yanayofanywa na kundi la Boko Haram hutokea maeneo yaliyo na waisilamu wengi kaskazini mwa nchi. Kundi hilo linataka sheria za kiisilamu kutumika katika nchi hiyo, ambayo watu wengi ni waumini wa kiksristo na ambao wengi wanaishi maeneo ya Kusini mwa nchi.
0 comments:
Post a Comment