KWA TAARIFA YAKO--WADOGO ZAKE UCHE WOTE WAFUATA NYAYO ZA WAZAZI ''WACHUNGAJI''
Pastor Uche akiwa na mdogo wake anayemfuatia Pastor Samuel Bruno. |
Uche ambaye alibarikiwa mwaka 2010 kuwa mchungaji kupitia Alleluia Ministry ya Afrika ya kusini, mdogo wake anayemfuatia Samuel Bruno ni mchungaji ambaye amefungua huduma yake jijini London nchini Uingereza ikifahamika kwa jina la Hopeway Ministries International, huku wadogo zake kama Miracle Bruno, Chisomi Bruno wenyewe wako nyumbani Nigeria na wazazi wao wakitumika katika makanisa mbalimbali wakifahamika kama wainjilisti hata Uche alithibitisha hilo wakati alipofanyiwa mahojiano na Wapo Radio Fm siku zilizopita.
MY GOD IS GOOD EVERYTHING DOUBLE DOUBLE
Wimbo huu ndio uliompa Uche tiketi ya kujiunga na Joyous mwaka 2009 baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Maduhva aliyekuwepo katika kanisa la Rhema North aliposikia mwimbaji huyo akiimba wimbo huo nakuupenda nakuamua kumtafuta mmoja wa viongozi wa kundi la Joyous bwana Lindelani Mkhize(choir master) ambaye aliamua kumwalika Uche kwenye mazoezi yao na kuanza kuufanyia mazoezi wimbo huo hatimaye kurekodiwa na Uche milango kuanza kufunguka nasasa anashiriki na waimbaji wengine wa kimataifa wa injili jukwaa moja.
Pamoja na hayo mwimbaji huyu lengo lake lilikuwa awe mwanasheria hakuwahi kuwaza kuja kuwa mwimbaji ingawa alipokuwa mtoto alikuwa akiimba kwaya ya watoto, amesema wazazi wake hawajawahi kumlazimisha kumwamini Mungu ama kuwa mwimbaji bali walikuwa wakimuombea mpaka Mungu alipomuonyesha wito wake katika maisha ambako anasema kwakweli ana kila sababu ya kumshukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri.
Wazazi wa pastor Uche. |
Uche akiwa na wadogo zake waishio Nigeria alipowatembelea mapema mwezi May mwaka huu. |
0 comments:
Post a Comment