Home » »

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUKUTANA IJUMAA HII

Wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake ijumaa hii wanatarajiwa kujumuika pamoja katika mkesha mkubwa wa maombi na maombezi unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa BCIC Mbezi beach uliochini ya Wapo Mission International na kiongozi wake askofu Sylvester Gamanywa.

Mkesha huo ambao unatarajiwa kuwa na vipindi mbalimbali vya kusifu na kuabudu pamoja na neno la Mungu pamoja na maombi umekuwa ukivutia maelfu ya wakazi wa jiji hilo kutokana na kile ambacho Mungu amekuwa akitenda kupitia watu wake.Ambapo maombi maalumu yatafanyika kwa watu wote hususani wanafunzi ambao wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani yao pamoja na kufeli katika mambo mbalimbali, watu wanaoteswa na vifungo mbalimbali vya shetani, yakiwemo majini na mambo mengi yafananayo na hayo.

Kati ya waimbaji watakaokuwepo ijumaa hii kwenye mkesha huo ni pamoja Emanuel Mgogo kutoka Mbeya, Masanja Mkandamizaji, Kikundi cha kusifu na kuabudu cha Mbezi beach BCIC na waimbaji wengineo, mkesha huo utaanza majira ya saa 3 usiku na kuendelea huku kituo cha Wapo Radio Fm kikirusha live mkesha huo.
Rais wa Wapo Mission International, askofu Sylvester Gamanywa akiwa katika moja ya ibada kituo cha Mbezi beach kutakofanyika mkesha huo.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog