ROSE MUHANDO AKAMILISHA ALBUM MPYA CHINI YA SONY MUSIC AFRIKA YA KUSINI
Kwa mujibu wa taarifa alizotoa mwimbaji huyo hii leo amesema amekamilisha nyimbo tatu zilizokuwa zimebakia katika kukamilisha album hiyo ya sauti ambayo hata hivyo hajaitaja jina. Mwimbaji huyo ambaye aliingia mkataba na kampuni hiyo ya kimataifa mapema mwaka jana, tayari amepata mafanikio makubwa kwenye medani ya muziki wa injili nchini tokea atoe album yake ya kwanza ya ''Mteule uwe Macho'' hadi yasasa ya ''Utamu wa Yesu''.
Hapana shaka kwamba album mpya itakuwa na kiwango kikubwa zaidi cha usikivu si kwenye sauti tu pia muziki wake utakuwa umerekodiwa kwenye viwango vikubwa kitu ambacho kitalifanya jina la Kristo lizidi kutangazwa si Tanzania tu bali maeneo mbalimbali duniani. Kila la kheri Rose Muhando.
Rose Muhando |
0 comments:
Post a Comment