MFALME WA R&B AFRIKA YA KUSINI AOKOKA, APOTEZA DILI YA KUFANYA KAZI NA MMAREKANI
Loyiso Bala mfalme wa R&B Afrika ya kusini aliyeamua kuokoka. |
Mwimbaji huyo aliyepewa jina la mfalme wa R&B nchini kwao, ameamua kuachana na uimbaji wa muziki wa nje ya kanisa na kuamua kumwimbia Mungu akitoa sababu nyingi ikiwemo aliyosema kwamba katika maisha yake amepata mafanikio makubwa sana ya muziki ikiwa pamoja na tuzo tano za SAMA na tuzo nyingine mbalimbali.
Ameimba mbele ya Will Smith, Oprah, zaidi ya mara nane kwenye kinyang'anyiro cha Miss SA, na mengineyo lakini katika hayo yote bado alikuwa akihisi kuna kitu hakikosawa ndani ya moyo wake na kitu chenyewe ni suala la kiroho jambo ambalo lilimfanya kwenda shule ya biblia ya Rhema Bible school ambako alikwenda kusomea kozi iitwayo ''Heart of Worship'' ambayo amesema ilimbadilisha haswa na kuona kabisa hakuna mwimbaji mwingine wa kumuimbia zaidi ya Mungu.
Loyiso ambaye ana miaka 30 sasa amesema hashangazwi na watu walivyoshangaa salamu hiyo licha ya kwamba walijua anazindua album ya gospel, amesema walijua ameimba album hiyo kwa ajili ya biashara lakini hawakujua ukweli kwamba sasa maisha yake yamebadilika kabisa na kuamua kumwimbia Mungu. Wakati hayo yakitokea mwimbaji huyo amepoteza nafasi ya kurekodiwa na mtayarishaji wa muziki nchini Marekani kama alivyokuwa akiomba maishani mwake itokee hivyo lakini imekuja kutokea wakati imani yake imebadilika na ujumbe wa nyimbo zake kumwelekea Mungu hali iliyofanya mtayarishaji huyo kuamua kuachana na mwimbaji huyo jambo ambalo hata hivyo mwimbaji huyo ajutii.
Mwimbaji huyu pia huwa anaimba na kundi la ndugu zake liitwalo Bala Brothers.
Haya ni baadhi ya maneno aliyonukuliwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kile kilichotokea maishani mwake
''The funny thing is at the time that I made this decision, I had to let go an opportunity to record with a US producer. For years I had been trying to get a US deal and when this particular guy came through it was a big deal for me.
He produced Jason Derulo, and all he needed was R400 000. But when I was in Scotland, with the Bala Brothers, I decided I wanted to make a gospel album. As I decided that, literally the following day, my manager called to say there was a guy in Kenya who was willing to pay for my trip to the US to record and I turned it down.
I knew that my heart was not in it anymore,I found greater purpose in doing Love Complete than go out there to be another stat,” he said.
0 comments:
Post a Comment