Home » »

KWA TAARIFA YAKO;--ZIJUE BARAKA ZINAVYOMIMINIKA KWA BAHATI BUKUKU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Photo: Ushanunua cd yake mpya?
Bahati Bukuku katika pozi. picha kwa hisani ya Ireene Mwamfupe.
                         
KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kwamba japo kwa ufupi fahamu baraka ambazo Mungu amembariki mtumishi wake ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili nchini aitwaye Bahati Bukuku, mwimbaji huyu ambaye ameachia album yake mpya ya 4 hivi majuzi inayoitwa ''DUNIA HAINA HURUMA'',ambayo tayari imeanza kufanya vyema mtaani na kwenye vituo vya radio.

Licha ya uimbaji Mungu ambao amekuwa akiwabariki wengi na nyimbo zake zenye ujumbe muafaka kwa jamii ni kwamba mwimbaji huyu anamiliki mali mbalimbali kama alivyoainisha mwenyewe alipozungumza na blog ya unclejimmytemu alisema ;-

Kwa sasa anamiliki Nyumba {4} alizo jenga mwenyewe,mbili Tabata Migombani,moja Bunju nyingine Mbezi beach.
Ana mashamba {4} Kitunda,Bunju,Kibaha na Mbeya.Mashamba hayo yana takribani ekari 2 mpaka 5.

Ana {Makarashi 2} yakusaga dhahabu mkoani geita.
Anamalizia Hotel yenye vyumba 38 mkoani geita,mwezi wa kumi na mbili mwaka huu inakwenda kufunguliwa rasmi,Hotel hii itaitwa Double B Hotel.

Pia yuko mbioni kufungua mgahawa (restaurant) karibu na hospital ya Regency mgahawa ambao utatoa huduma zote za chakula.

Hakuishia hapo Bahati aliweka bayana mambo mengine pamoja na namna alivyozipata mali hizo;-
Iko siri katika kulima nakufuga.Mimi nimezaliwa kwenye familia inayopenda kulima na kufuga.Nilianza kulima Mahindi na Karanga baadae nikaingia kufuga kuku.
Kwa sasa ninakuku wengi sana ninaofuga hapo Kibaha,asikudanganye mtu kilimo kinalipa sana nandio mana sipatikani mjini mara kwa mara nipo shamba nikicheza na Jembe.
Hizo ni baadhi ya baraka ambazo Mungu ameendelea kuzimimina kwa Bahati Bukuku aliyetamba na album kama ''NI NYAKATI ZA MWISHO'', ''NANI AITIKISE DUNIA'', NIMESAMEHEWA DHAMBI SIO MAJARIBU nasasa album mpya ''DUNIA HAINA HURUMA'' ambayo wimbo wake unatarajiwa kutengenezewa filamu na mchakato umekwishaanza.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog