NYOTA WA MUZIKI WA INJILI MAREKANI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI
Mwimbaji anayetamba na wimbo wake maarufu "Break every chain" Tasha Cobbs wa nchini Marekani amefiwa na baba yake mzazi askofu Fritz Cobbs katika taarifa ambayo ilitolewa na mwimbaji mwingine wa injili nchini humo James Fortune kupitia mitandao ya kijamii kwakuwataka wapenzi wa muziki wa injili kumkumbuka katika maombi mwimbaji huyo kwakuwa amefiwa na baba yake mzazi.
Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.
0 comments:
Post a Comment