Watu wawili wanashikiliwa na polisi nchini Tanzania
baada ya kukamatwa na shehena ya meno ya tembo katika bandari ya Dar es
Salaam, waliyokuwa wakisafirisha kiharamu maafisa wa nchi hiyo
wamesema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa
Wizara ya Maliasili na Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha amesema meno
hayo yapatayo 81 yana uzito wa kilo 303.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya
tembo ni mapya ikiwa na maana yametokana na tembo 41 waliouawa ndani ya
mwezi mmoja uliopita.
Naibu Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania
Lazaro Nyalandu amesema mauaji ya tembo yameongezeka nchini humo baada
ya operesheni ya kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni
Tokomeza" kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za
binadamu.
Mapema wiki hii Naibu Waziri huyo amesema tembo
wapatao 60 wameuawa kati ya mwezi Novemba na Decemba ikilingalishwa na
tembo wawili waliouawa mwezi Octoba.
0 comments:
Post a Comment