MAN UNITED MWAKA WA TABU, YATOLEWA KOMBE LA FA, YAPIGWA 2-1 NA SWANSEA
MIKOSI
imeendelea kwa kocha David Moyes, baada ya Manchester United kufungwa
mabao 2-1 na Swansea katika Raundi ya tatu ya Kombe la FA na kutolewa.
Bao
lililoizamisha United iliyocheza pungufu ya mchezaji mmoja lilifungwa
na Wilfried Bony dakika ya mwisho na Mashetani Wekundu wa wanatolewa
katika raundi ya tatu kwa mara pili ndani ya miaka 30.
Javier Hernandez aliisawazishia United dakika ya 17 baada ya Wayne Routledge kuifungia Swansea bao la kuongoza dakika ya 12.
Bony akiruka dhidi ya mabeki wa United kufunga
Katika
mchezo mwingine, Liverpool imeifunga mabao 2-0 Oldham na kusonga mbele
mabao ya Iago Aspas dakika ya 54 na Tarkowski aliyejifunga dakika ya 84.
Bao la kwanza: Iago Aspas akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
0 comments:
Post a Comment