...................................................................................................................
...............................
MKAZI wa Kijiji cha
Ihowanza wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa John Nwali (40) akutwa amekufa baada ya kutoweka nyumbani kwake kwa
wiki moja mara
baada ya shamla shamla
za kuuaga mwaka mpya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo leo alipokuwa akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake.
Alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Januari 9 majira ya saa 1 jioni mwaka huu katika Kitongoji cha
Ihowanza Kata ya Ihowanza Tarafa ya Malanali Wilaya ya Mufindi.
Alisema mwili wa
mkazi huyo ulikutwa
janurai 9 majira ya jioni huku mwili
wake ukiwa umeharibiwa vibaya na baadhi
ya viungo vyake kuliwa na mbwa na kuwa
jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi zaidi juu ya kifo
hicho.
0 comments:
Post a Comment