Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kulia akieleza jinsi
ambavyo mkoa ulivyotekeleza ilani ya uchaguzi kwa mwaka 2013
SERIKALI ya mkoa wa Iringa leo
imetoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa mwaka 2013
huku ikijivunia mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa.
Akitoa taarifa hiyo leo mbele ya
wanahabari mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema
kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo mkoa wa Iringa unajivunia
ni katika sekta ya elimu, miundo mbinu, kilimo ,afya na nyingine
nyingi.
Kwani alisema kuwa mkoa umepiga
hatua katika ujenzi wa nyumba za walimu katika Halmashauri zote za
mkoa wa Iringa lengo likiwa ni kuendelea kuboresha kiwango cha
elimu katika mkoa.
Akielezea kuhusu sekta ya afya
alisema kuwa hadi sasa Hospital mbili zinaendelea kujengwa katika
manispaa na Kilolo pia vituo vya afya na nyumba za watumishi wa
afya ikiwa ni pamoja na kuendelea kusambaza dawa katika vituo vya
afya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema pia kumekuwepo na ufuatiliaji wa huduma zinazotolewa katika vituo hivyo na Hospital . |
0 comments:
Post a Comment