HISTORIA YA MWANAMUZIKI WA INJILI EPHRAIM SEKELETI MUTALANGE
|
Ephraim Sekeleti |
Ephraim Sekeleti Mutalange ni muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia, alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia. Alimaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Kalulushi mwaka 2001.
Ephraim
ni mtoto wa pili toka mwisho kati ya watoto sita, aliingia kwenye
muziki wa injili tangu akiwa kinda huku alifundishwa kupiga kinanda na
mmishonari alipokuwa bado mdogo. Mama yake anasema “
Ephraim alikuwa ni mtoto aliyekuwa wa kelele nyingi”. Yeye pamoja na
dada zake waliimba kanisani wakitumia kinanda na huko alipata uzoefu
katika uimbaji na upigaji wa kinanda. Baadaye alijiendeleza katika
uimbaji kwenye kikundi kilichojulikana kwa jina la “Virtue for Christ” na aliimba katika kikundi hicho kwa muda wa miaka miwili.
|
Ephraim akiimba katika ibada ya kanisa la redeemed christian nchini Australia |
Mwaka
2002 akiwa na kiu ya kurekodi album yake, Aliamua kujitoa muhanga
kwenda Afrika ya Kusini kwa kutumia kiasi kidogo tu cha pesa alichokuwa
nacho, nia ilikua ni kurekodi album yake ya kwanza. Pamoja na jitihada
hizo, baada ya kufika nchini Afrika ya Kusini alijikuta anaweza kurekodi
nyimbo mbili tu kati ya album nzima. Hivyo akaamua kujiingiza katika
Theater ya Pretoria
na ndipo akapata fursa ya kuimba mbele ya Rais wa Afrika ya Kusini.
Nafasi nyingi ziliendelea kujitokeza zilizomsababishia kutaka kuacha
kuendelea na muziki wa injili ili aimbe miziki ya kidunia, lakini akawa
muaminifu kuendelea na uimbaji wa injili. Mlango ulifunguka kumruhusu
kurekodi album ya kwanza iitwayo Temba Baby“(Mtoto wa Miujiza)”.
Baada
ya kurekodi, na kuuza nakala za kutosha za album hiyo ya Temba boy, kwa
mafanikio ya hiyo kazi Ephraim aliamua kurudi nyumbani kuwekeza ile
fedha. aliona awekeze zaidi kwenye ya album yake ya pili iliyopata
mafanikio makubwa iliyoitwa Limo Ndanaka. Hi album imefanya vizuri
kwenye chati mbalibali za muziki wa injili. Ephraim akiwa nje ya Zambia ameimba katika nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Zimbawe na Australia.
|
Ephraim akiwa na mkewe Faith Mutalange
|
Alisema anafurahi akiona watu wasiokuwa na tumaina la Kristo wakianza kuwa na matumain, Licha ya kufanya muziki wake nchini Zambia amewahi kuja nchini Tanzania na kurekodi album yake nzima kwa Lugha ya Kiswahili. Moja kati ya Nyimbo zake zinazotamba hapa nchini ni pamoja na
|
Binti wa Ephraim
|
1. Uniongoze
2. Baraka Zako
3. Huu Mwaka
Ephraim
hajui Kiswahili fasaha na nyimbo zake hizo alifundishwa kuziimba kwa
lugha ya Kiswahili na Mchungaji ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za
Injili kutoka Tanzania Ency Mwalukasa. Ephraim amesema ataendelea
kuhubiri kwa njia ya uimbaji kwa sababu imempa changamoto zilizomuinua.
Licha ya uimbaji Ephraim amefunga ndoa na Faith Chelishe na wamejaliwa
kupata mtoto mmoja wa kike
|
Ephraim na Faith
|