KWAYA YA KWETU PAZURI WAKO NCHINI ZAMBIA

Ambassadors of Christ wakiimba katika tamasha la pasaka jijini Mbeya mapema mwaka huu.

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka Kigali nchini Rwanda maarufu kama Kwetu Pazuri wapo nchini Zambia kwa ziara ya siku tano ukiwa ni mwaliko wa kanisa la Wasabato Libala la jijini Lusaka ambapo kwaya hiyo itashiriki katika maonyesho makubwa matatu nchini humo yanayotarajiwa kuanza siku ya jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo matamasha hayo ambayo yatakuwa na viingilio ili kusaidia ujenzi na huduma ya kanisa la Libala yatafanyika katika ukumbi wa Blessing centre kisha uwanja wa mpira wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola na kumalizia katika ukumbi wa New Government complex siku ya tarehe 2. Kwaya hiyo ambayo ilipata umaarufu sana nchini Tanzania mwaka 2011 kutokana na album yao ya Kwetu pazuri, imekuwa ikipata mialiko katika nchi mbalimbali za Afrika ambako wameonyesha kiu ya kuwaona waimbaji hao.

Ambapo kwa mwaka huu Ambassadors walishiriki tamasha la pasaka nchini Tanzania, tamasha ambalo hata hivyo liliwaweka katika wakati mgumu na makanisa ya kisabato nchini kutokana na kukubali kushiriki tamasha hilo, lakini pia walikuwa nchini Uganda pamoja na Goma nchini Kongo ambako wameshiriki katika matamasha mbalimbali ya kusaidia huduma za makanisa ya Kisabato.

Uwanja wa Levy Mwanawasa ulipo Ndola nchini Zambia,ambapo Ambassadors of Christ wataimba siku ya jumapili.

BINTI ATISHIWA KUCHINJWA NA KUSILIMISHWA KWA NGUVU NIGERIA

Hajja ©Reuters/Joe Brock
"Nilipolia walinipiga, na nilijaribu kuongea pia walinipiga. Waliniambi aninlazima nisilimu kuwa Muislamu ili wasiniue". Hajja anasimulia, binti mwenye umri wa miaka 19, ambaye amepona kwenye mikono ya kundi la kigaidi lenye uhusiano na al-Qaeda, Boko Haram nchini Nigeria.
Milima ya Gwoza ndiko ambako kijiji cha binti Hajja kinapatikana, ambapo kuna siku alikuwa kwenye shughuli za kawaida alipotekwa na kundi hilo, na kulazimishwa kuzunguka nalo kwa miezi mitatu huku akiwapikia na kuwafulia nguo zao.
Katika ushuhuda ambao ameueleza kwa shirika la habari la Reuters, Hajjaa anasema kuwa. licha ya kwamba hakubakwa, ila alikuwa akiteswa vibaya sana na kulazimishwa kuachana na Ukristo, ili apate kuishi, jambo ambalo alikuwa akipingana nao kwa nguvu, hatua ambayo ilimfanya mmojawapo wa watekaji kumbembeleza ili asiuawe kwa kuchinjwa, ambapo siku moja kabla tu hajauwawa ilimbidi akubaliane nao na kuapishwa - na kisha kulazimishwa kusoma Quran.
Kati ya mayeso ambayo ameyapata, Hajja anaeleza kuwa alikuwa ni mtu wa kufua na kupika, na kama hakuwa akifanya hizo shughuli basi alilazimishwa kubeba silaha zao, na kisha siku moja hatosahau ni pale ambapo walimfanya chambo/mateka mbele ya wanajeshi wa serikali ili wasidhurike wala kukamatwa.

CHRISTINA SHUSHO ALIVYOWEKA MAMBO SAWA CCC JUMAPILI

Siku ya jumapili tarehe 24 November, 2013 katika Ukumbi wa Kanisa la CCC Upanga Mwanamuziki wa injili aliyejijengea jina katika ukanda wa Afrika Mashariki na Mwanamuziki anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi kuliko wanamuziki wengine wa injili inchini Tanzania Christina Shusho amefanya Live Recording ya aina yake katika Ukumbi huo.

Live Recording hiyo ilianza majira ya saa 12 ilikuwa nikiwango cha kimataifa na Iliandaliwa kwa ustadi Mkubwa kulinganisha na matamasha mengine ya Injili hapa Tanzania. Christina Shusho katika Nyimbo zake hizo pia alifanya Collabe na wanamuziki wengine wa injili hapa Tanzania kama Upendo Kilahiro pamoja na Joshua Mlelwa. Mgeni rasmi katika Tamasha hili alikuwa Mhe. Bernad Membe waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Waziri hiyo akizungumza katika tamasha hilo alisema ipo haja ya vijana wa kitanzania kumcha Mungu ili kuweza kuja kuwa viongozi wa nyanja mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa hapa Tanzania.

Christina Shusho akiwa sawa stejini.
Christina na Upendo Kilahiro wakiimba pamoja Thamani ya wokovu wangu.
Waitikiaji wa Christina Shusho wakienda sawa.
Mgeni wa heshima mheshimiwa Benard Membe akizungumza na waumini waliofika tamashani.
Christina Shusho akienda sawa na kundi la The Voice.
MC no 2 watukio, unclejimmy temu akienda sawa.
Mpiga Saxaphone nambari One Nchini Uganda Isaiah akihudumu.
Shetani aliipata, maana thamani ya wokovu ilikuwa level nyingine.

Vijana wakisebeneka wakati wa tamasha.
Samuel Yona, aliyeandaa na kuongoza muziki wa mwanamama Christina Shusho.
Upendo Kilahiro na Christina Shusho.
Kamati iliyoandaa tamasha hilo.

ANGALIA PICHA ZA SHANGILIENI KWAYA WAKIWA AFRIKA YA KUSINI KIHUDUMA

Kwaya ya Tumaini Shangilieni toka St.James Kaloleni Arusha inatarajiwa kuwasili siku ya leo ikitokea nchini Afrika ya kusini ambako ilikwenda katika kanisa la Anglican kitongoji cha Tembisa jijini Johannesburg kihuduma. Kwaya hiyo ambayo iliondoka na ndege ya Fastjet siku ya ijumaa, imefanikiwa kufikia lengo lililowapeleka nchini Afrika ya kusini kumuhubiri Kristo.

Wakati huohuo taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba kwaya hii inatarajiwa kuwepo usharika wa Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam siku ya tarehe 8 mwezi ujao katika kuwasindikiza kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ambayo itakuwa ikisherehekea miaka 25 ya kwaya yao tangu ilipoanzishwa.


Taarifa kamili na picha nyingine zitawajia kupitia hapa hapa GK. Kwa leo pata japo kwa kifupi
Mawinguni mwe!
Muonekano wa jiji la Johannesburg kutokea juu karibu na uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Mwenyekiti wa Tumaini Dkt. Emanuel Mtangoo na wanakwaya wengine wakizungumza na mwenyeji wao mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Safari ya kuelekea kanisani.
Usharikani Tembisa.
Waimbaji wa Tumaini wakiwa kanisani siku ya jumapili.

YAYA TOURE AITISHIA AMANI CHELSEA, AWAAMBIA REKODI YAO IKO HATARINI

KIUNGO Yaya Toure anaamini Manchester City inaweza kuvunja rekodi ya mabao ya msimu katika Ligi Kuu England msimu huu.
Kiungo huyo wa nguvu amempa jeuri kocha Manuel Pellegrini juu ya uwezo wa kushambulia unaoleta matumaini ya taji kwa kusema rekodi ya Chelsea iko hatarini.
Kocha Carlo Ancelotti akiwa na kikosi mariadi msimu huu 2009-10 aliiwezesha Chelsea kufunga mabao 103 na kutwaa taji misimu minne iliyopita.
Jitu la nguvu: Yaya Toure (kushoto, akipambana na Paulinho wa Spurs, amesema City inaweza kuvunja rekodi ya mabao
Six of the best: Sergio Aguero netted twice in City's rout of Tottenham on Sunday
Mabao sita: Sergio Aguero alifunga mabao mawili City ikiifumua Tottenham Jumapili
Put your hands up: Chelsea netted an incredible 103 goals on their way to winning the Premier League in 2010
Inua mikono juu: Chelsea ilifunga mabao 103 wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 2010

Na baada ya timu ya Pellegrini kufikisha mabao 34 wakiifunga sita Spurs Jumapili, Toure amesema lengo ni kuvunja rekodi hiyo.
Alipoulizwa kwamba inaezekana kuipiku rekodi ya Chelsea, alijibu: "Natumaini hivyo — tuna washambuliaji. Watu wawili mbele (Alvaro Negredo na Sergio Aguero) hawa watu huwezi kuamini. Wanajiamini sana.
"Lakini si kwa sababu ya wachezaji hao wawili tu. Ni timu nzima. Tunashambulia sana na washambuliaji wote wanafurahia hii. Hata (Edin) Dzeko na (Stevan) Jovetic.
"Timu inaelekeza nguvu zake katika kushambulia. Ni babu kubwa. Na unaposhinda kama tulivyofanya kwa Tottenham ni nzuri. Ni washindani wa kweli katika mbio za taji la Ligi Kuu mwaka huu,".
Out of action: But even Edin Dzeko is enjoying life at goalscoring City at the moment, claims Toure
Nje ya Uwanja: Lakini hata Edin Dzeko anafurahia maisha namna ambavyo City inafunga mabao, amesema Toure

MAVETERANI KENYA NA BARA KUKUMBUSHIA CHALLENGE YA ENZI HIZO, HUO MUZIKI WA HARAMBEE USIUPIMIE, KUNA MAHMOUD ABBAS, PETER DAWO, J J MASIGA, JUA CALI NA KADENGE, STARS…

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
WACHEZAJI wa zamani wa Kenya ‘Wazee wa Kazi’ wametaja kiksi cha nguvu ambacho kinamenyana na wakongwe wenzao wa Bara kutia nakshi michuano ya mwaka huu ya Challenge.
Kikosi hicho chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao waliwika Harambee Stars enzi zao.
Wazee wa Kazi; Wachezaji wa zamani wa Harambee Stars

Kikosi hicho ni; Mohammed Abbas (kipa), John Busolo (kipa), Josphat Murila (beki), George Sunguti (mshambuliaji), Austin Oduor (mshambuliaji), Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo (mabeki), Allan Thigo (kiungo), Joe Kadenge (mshambuliaji), Tobias Jua Kali Ochola (beki), Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu (mabeki), Paul Ochieng’ (beki), Peter Dawo (mshambuliaji), Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga (washambuliaji), Paul Onyiera (kiungo), Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, James Siang’a (makipa), Abdul Baraza, Ricky Solomon, John Bobby Ogola, James Nandwa (washambuliaji), Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya na David Ochieng’.
Tanzania Bara bado haijataja kikosi chake kitakachokuja Nairobi na hadi jana hakukuwa na taarifa za hata kuanza mazoezi.

BARA KUJIFUA STIMA PAMOJA NA SUDAN, ETHIOPIA LEO

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
TIMU zinazoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ambayo mwaka inafanyika hapa Nairobi, Kenya ikidhaminiwa na Serikali, zitafanya mazoezi katika viwanja vijnne tofauti leo.    
Viwanja hivyo ni Stima Club, Chuo Kikuu cha Strathmore, Uwanja wa City Stadium Ktuo cha Kimataifa cha Michezo cha Moi (MISC), Kasarani.
Uchovu umeisha; Kocha wa Bara, Kim Poulsen leo atakiongoza kikosi chake mazoezini kwa mara ya kwanza Nairobi, baada ya kuwasili jana. Chini, kikosi cha Stars kikiwasili Nairobi jana usiku.

MISC, Kasarani umetengwa maalum kwa ajili ya wenyeji, Kenya, Harambee Stars, wakati Tanzania Bara, Sudan na Ethiopia watafanya pamoja kwenye Uwanja wa Stima.
Rwanda, Sudan Kusini na Burundi watatumia viwanja viwili vya Strathmore, huku Somalia, Zanzibar na Eritrea wakitumia mwingine na mabingwa watezi Uganda na Zambia watatumia Uwanja wa City.

900 waliuawa katika vita dhidi ya M23

Jeshi la congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei.
Wanajeshi wa DRC
Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700 waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Wanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa kwenye makabiliano hayo.
Pia wapiganaji 72 wa Rwanda na wapiganaji 28 wa Uganda waliuawa.
Mwanzoni mwa mwezi huu, waasi wa M23 walitolewa na jeshi la serikali iliyoungwa mkono na kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 wa Umoja wa Mataifa lakini serikali ya Congo na waasi walikosa kuelewana kuhusu mpango wa baadae wa amani.
Waasi wa M23 walisitisha vita na kujisalimisha baada ya jeshi la DRC kwa ushirikiano na wanajeshi wa UN kupigwa vita vikali na kuwaondosha katika maeneo waliyokuwa wameyateka.
Maelfu ya wakaazi wa Mashariki mwa DRC walilazimia kukimbilia nchi jirani ya Uganda kutafuta hifadhi wakati kundi hilo lilipokuwa linaendesha uasi wao na hata kuuteka mji wa Goma kwa muda.
Kudni la M23 lilifanya vitendo vya kikatili dhidi ya watu wa Mashariki mwa DRC ikiwemo ubakaji na kuwatumia watoto kama wapiganaji.

BALOTELLI AZUA LINGINE ITALI BAADA YA KUTWEET "THIS IS THE END"

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewachangasha tena mashabiki wake leo baada ya kutweet 'this is the end' (huu ni mwisho) saa kadhaa baada ya kukosa penalti AC Milan ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa.
Mshambuliaji huyo hatari, alitweet ujumbe huo Kiingerezamajira ya saa 11 Alfajiri kwa sa za kwao katika akaunti yake ya @finallymario.
Pamoja na hayo, saa sita baadaye akatuma ujumbe mwingine wa tweet Kitaliano, uliosomeka: ‘Forza Milan comunque e sempre.’ ambao Kiingereza ni 'Go on Milan, no matter how and forever'.
Mwisho wa barabara? Mario Balotelli alikosa penalti timu yake AC Milan inayosuasua ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa
What does he mean? Balotelli tweets after AC Milan's draw with Genoa
Anamaanisha nini? Balotelli ametweet baada ya sare ya AC Milan na Genoa
Turn around? Balotelli later tweeted his support for Milan a few hours later
Spot of bother: Balotelli misses a penalty against Genoa
Balotelli akipiga penalti aliyokosa
No joy: Balotelli has missed two penalties this season
Hakuna furaha: Balotelli amekosa penalti mbili msimu huu
Down and out: Mario Balotelli looks dejected as AC Milan fail to win again
Down and out: Mario Balotelli looks dejected as AC Milan fail to win again

MAN CITY YAIFUMUA SPURS 6-0, JESUS NAVAS ALIFUNGUA BIASHARA NZURI SEKUNDE YA 14 TU NA AKAIFUNGA DAKIKA YA 90

BAO la mapema sekunde ya 14 la Jesus Navas lilifungua biashara nzuri leo Man City ikiibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Tottenham.
Winga huyo wa Hispania, Navas alifunga bao la pili la mapema msimu huu kufuatia makosa ya kipa wa Spurs, Hugo Lloris.
Sandro alijifunga dakika ya 34 kuipa bao la pili timu ya Manuel Pellegrini kaba ya Sergio Aguero kufunga mawili dakika za 41 na 51, Alvaro Negredo akaongeza dakika ya 56 na Jesus Navas akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 90.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Pantilimon, Zabaleta, Demichelis, Nastasic/Lecsott dk45, Clichy, Toure, Fernandhino, Navas, Negredo, Nasri/Milner dk77 na Aguero/Garcia dk69.
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Kaboul, Vertonghen, Sandro, Lennon, Holtby/Adebayor dk45, Paulinho/Dembele dk60, Lamela na Soldado.
Bao la mapema: Jesus Navas aliifungia Man City bao la mapema sekunde ya 14 dhidi ya Tottenham
Ahead: Navas jumps over the corner flag after putting Man City into an early lead
Ahead: Navas jumps over the corner flag after putting Man City into an early lead
At the double: Sandro deflects the ball into his own net following Alvaro Negredo's volley
At the double: Sandro deflects the ball into his own net following Alvaro Negredo's volley
Strike: Hugo Lloris watches on as Sergio Aguero extends Man City's lead just before half-time
Strike: Hugo Lloris watches on as Sergio Aguero extends Man City's lead just before half-time
Exquisite: Negredo shoots after an excellent turn to get the better of Spurs defender Michael Dawson
Exquisite: Negredo shoots after an excellent turn to get the better of Spurs defender Michael Dawson
Team effort: Negredo celebrates with team-mates Aguero and Samir Nasri after scoring Man City's fifth goal
Team effort: Negredo celebrates with team-mates Aguero and Samir Nasri after scoring Man City's fifth goal
Hit for six: Jan Vertonghan slides in as Navas slots home City's sixth goal in the last minute
Hit for six: Jan Vertonghan slides in as Navas slots home City's sixth goal in the last minute
Battle: City frontman Aguero holds off a challenge from Tottenham midfielder Sandro during Sunday's clash
Battle: City frontman Aguero holds off a challenge from Tottenham midfielder Sandro during Sunday's clash
Stretching: Aguero attempts to chip the ball over Hugo Lloris but sees his effort saved by the French goalkeeper
Stretching: Aguero attempts to chip the ball over Hugo Lloris but sees his effort saved by the French goalkeeper
Missing out: Joe Hart watches on from the bench as City run riot against Tottenham
Missing out: Joe Hart watches on from the bench as City run riot against Tottenham

KAMPUNI ya Simba Logistic Equipment Supply yazindua kifaa cha kuzimia moto kwa kurusha kiitwacho B

kifaaa-1 _DSC0036 - Copy-1 _DSC0041 _DSC0054 - CopyKAMPUNI ya Simba Logistic Equipment Supply hivi karibuni ilizindua kifaa cha kuzimia moto kwa kurusha kiitwacho Bonex ambacho vinatumia kuzimia moto katika majumba, magari na sehemu nyinginezo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simba Logistic Equipment Supply Co Limited, Fareed Nahdi alisema kuwa vifaa hivyo ni rahisi kutumika katika matukio mbalimbali ya kuzimia moto.
Alisema kuwa havihitaji matengezo ya mara kwa mara kwa kuwa vikinunuliwa vinatumika kwa mara moja kwa tukio moja.
Alisema kuwa ni vifaa ambavyo ni rahisi kubebeka na kutumika katika mazingira yoyote kutokana na udogo wake ambao unaumuhimu mkubwa katika kuzima moto.
“Hii ni aina mpya ya uzimaji  moto kwa kutumia vifaa hivi muhimu ambapo ukitofautisha na vifaa vingine ambapo kunakuwa kuna maelekezo mengi ya kufuata lakini hiki unarusha tu hivyo hata watoto wanaweza kutumia”alisema Nahdi.
Alisema kuwa hakina madhara kama vile moshi wala aina nyingineyo ya madhara na kinasaidia harakati za uokozi wa wat.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga aliyekuwepo kushuhudia uzinduzi huo alisema kuwa kifaa hicho kinaweza kusaidia zaidi hata katika kuzima motoo wa magari.
Alisema kuwa wenye magari wanapaswa kwua na kifa hicho kwa kuwa ni rahisi kutumika pia.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog