DK SLAA KUZINDUA KESHO KAMPENI ZA CHADEMA UCHAGUZI MDOGO KALENGA, CCM KUANZA JUMAPILI
Dk Slaa |
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa kesho
Jumamosi atazindua kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wilayani Iringa
katika kijiji cha Kalenga.
Kwa
upande wao Chama cha Mapinduzi (CCM) kitanzaa kampeni zake keshokutwa Jumapili katika
kijiji cha Mseke wakati kikiendelea na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni
hizo.
Uchaguzi
huo unakishirikisha chama kingine cha Chausta kilichomsimamisha Richard Minja
kupeperusa bendera yake.
CCM
kwa upande wao imemsimamisha, Godfrey Mgimwa, huku Chadema ikiwa imemsimamisha
Grace Tendega.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa,
Pudenciana Kisaka, jimbo la Kalenga lina jumla wapiga kura 85,051.
Akizungumza Katibu wa Chadema Iringa Vijijini, Felix Nyondo alisema Dk Slaa atawasilia
mjini Iringa kwa gari mapema kesho katika mapokezi yatakayohusisha msafara
mkubwa wa magari na pikipiki katika eneo la Ndiuka mjini hapa.
Mbali
na Dk Slaa, Nyondo alisema wengine watakaokuwepo kwenye uzinduzi wa kampeni
hizo ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Leman na viongozi mbalimbali wa chama
hicho.
Alisema
baada ya uzinduzi huo, Chadema itaendelea na kampeni za kila siku na kwa mujibu
wa ratiba yao, kila siku watakuwa wakifanya mikutano 39.
Nyondo
alisema katika kampeni hizo Chadema itatumia helkopta (chopa) tatu, magari 56
na pikipiki 80.
Alisema
vyombo hivyo vya usafiri vitagawanywa katika kata zote 13 za jimbo hilo ili
kufanikisha shughuli nzima ya kampeni zao.
0 comments:
Post a Comment