DOKII,NYAMIDELA,MASCO NA EZENICE KUPAMBA KAMPENI ZA UCHAGUZI KALENGA
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Aliyekuwa msanii maarufu wa
maigizo ya kibongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ambaye
kwa sasa anajishughulisha na sanaa ya muziki hasa katika mambo ya siasa ameahidi
kuwepo mkoani Iringa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge
Dokii aliyasema hayo juzi
wakati aliposhiriki uzinduzi wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika katika kijiji cha
Kaning’ombe kilichopo jimbo la Kalenga
wilaya ya Iringa vijijini
msaani huyo alisema
atashiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni humo huku akiahidi katika kampeni hizo kusimama kwenye majukwa ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) kumpigia kampeni mgombea wake, Godfrey Mgimwa.
Kwa
upande wake msanii anayeshughulika na kazi za chama cha mapinduzi ccm
mkoa wa Iringa Damasi Masonda (Nyamidela) ambaye kwa sasa anatamba na
wimbo wa Godfrey Mgimwa washa moto kalenga alisema kuwa yeye kama msanii
anayekitumikia chama hicho atahakikisha anafanya kampeni ya kumnadi
Mgimwa katika jimbo lote la kalenga.
Nyamidela
ambaye alishawahi kuzunguka katika kampeni za urais mwaka 2010 amesema
kuwa moto alioufanya katika kampeni hiyo na kampeni za uchaguzi mdogo
wa udiwani mkoa wa Iringa ndio atakao washa katika jimbo la kalenga.
aidha
katika kampeni hizo wasanii wengine mkoani humo wanaotarajia kumnadi
mgombea Mgimwa ni msanii anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mgata
(Masco) ambaye anatamba kwa kibao cha maisha magumu kijana pambana
pamoja na ezekiel Nice (Ezenice) anayeondoka kwa nyimbo za mchiriku
huku akitamba kwa wimbo wa CCM chama bora.
uchaguzi huo
utakaofanyika Machi 16, mwaka huu umetokana
na aliyekuwa mbunge wake Dk William Mgimwa
kufariki dunia Januari 1, mwaka huu,
Katika uchaguzi huo mgombea
wa ccm Godfrey Mgimwa atapambana na wagombea wa vyama viwili vya siasa ambavyo ni
Chadema kilichomsimamisha mgombea Grace Tendega na Chausta kilichomsimamisha
Richard Minja.
0 comments:
Post a Comment