CCM NJOMBE NA IRINGA WALAANIA VURUGU ZA CHADEMA WATAKA WANANCHI WACHAGUE CCM, FILIKUNJOMBE AWAFUNDA NJOMBE , JESHI LA POISI LAONYA WATAKAOFANYA VURUGU KESHO KUKIONA
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza katika mkutano huku mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe akimsikiliza
............................................................................................................................
Kwa upande wake Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe kimeeleza kusikitishwa na vurugu mbali mbali zinazojitokeza katika kampeni za udiwani kata ya Njombe mjini baada ya wafuasi na viongozi wa Chadema kuwapiga wananchi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin alisema kuwa siasa inayofanywa na wana Chadema kwa Njombe mjini ni siasa ya kinyama na kuwa ilipendeza kwa vyama vya siasa kushindana kwa sera na hoja badala ya kushindana kwa vurugu .
HIvyo alisema kuwa ili CCM kuendelea kutimiza ahadi zake na kuongoza kata hiyo ni wajibu wa wananchi wa Njombe kuchagua mgombea wa CCM badala ya kuwasikiliza wafuasi hao wa Chadema kutoka nje ya Njombe ambao wapo kwa ajili ya kutaka kuvuruga uchaguzi huo.
Huku mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwataka wana Njombe mjini kutokubali kata hiyo ya Njombe mjini kuchukuliwa na vyama vya upinzani na kuwataka kuchagua chama cha mapinduzi.
Filikunjombe alitoa kauli hiyo wakati wa kumnadi mgombea udiwani wa CCM katika kata hiyo ya Njombe mjini na kuwa Wilaya ya Ludewa na Njombe ni wilaya majirani na kuwa masilimali za Ludewa ambazo ni makaa ya mawe na Liganga si tu ukombozi kwa wana Ludewa ni ukombozi wa mkoa wa Njombe na Taifa hivyo kuwataka vijana kuendelea kuwa na imani na serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete ambae katika utawala wake watanzania wanashuhudia miradi hiyo mkikubwa inaanza.
Alisema kuwa uchumi wa Njombe na Ludewa baada ya kuanza kwa miradi hiyo utakuwa zaidi kutokana na vijana wengi kupata ajira katika miradi hiyo.
0 comments:
Post a Comment